Tuesday, May 6, 2014
MKE AZIRAI BAADA YA KUHUKUMIWA MIAKA MITANO JELA YEYE NA MUMEWE LIVE.
Do you like this story?
Watu wawili wa familia moja Frank Charles na mkewe Asia
Khamis wamehukumiwa kifungo cha miaka mitano jela au kulipa faini
ya shilingi milioni moja kila mmoja kwa kosa la kukutwa na madawa ya kulevya
aina ya bangi.
Hakimu wa mahakama ya
wilaya ya Mbeya Maria Batulaine amewatia hatiani wanandoa hao baada ya
kuridhishwa na ushahidi usio shaka wa mashahidi wanne wa upande wa mashitaka.
Imedaiwa na Mwendesha
mashitaka wa Serikali Juliana William amesema kuwa washitakiwa hao walikutwa na
kete 100 za bangi Novemba 19 mwaka jana eneo la Makunguru Jijini Mbeya baada ya
upekuzi wa Polisi.
Baada ya kusikiliza
pande zote mbili aliwapa washitakiwa nafasi ya kujitetea ambapo walisema kuwa
wana watoto wawili mmoja akiwa darasa la nne na mwingine akiwa kidato cha tatu
hivyo kuiomba mahakama kuwaangalia kwa jicho la huruma kwa kuwa hilo ni kosa
lao la kwanza.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MKE AZIRAI BAADA YA KUHUKUMIWA MIAKA MITANO JELA YEYE NA MUMEWE LIVE.”
Post a Comment