Tuesday, May 6, 2014
TFF KUANZISHA MFUKO WA MAENDELEO, TENGA NDIYE MWENYEKITI.
Do you like this story?
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF) limeazimia kuanzisha Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu Tanzania (TFF
Development Trust Fund).
Uamuzi wa kuanzisha mfuko huo
umepitishwa katika kikao cha Kamati ya Utendaji ya TFF iliyokutana Mei 3 mwaka
huu jijini Dar es Salaam ambapo madhumuni yake ni kutafuta vyanzo vya
rasilimali za kuendeleza programu za mpira wa miguu Tanzania.
Mfuko huo utakaokuwa chini ya
uenyekiti wa Rais aliyepita wa TFF, Leodegar Tenga utatafuta rasilimali za
kuendeshea michuano ya Taifa na kimataifa ya wavulana na wasichana kwa vijana
wenye umri chini ya miaka 13, 15, 17 na 19.
Pia kuendeleza maeneo ya ardhi kote
Tanzania ambayo ni mali ya TFF kwa kujenga vituo vya michezo (sports centres),
kutafuta rasilimali za kutoa mafunzo kwa makocha, marefa, madaktari wa tiba ya
michezo na viongozi (administrators).
Majukumu mengine ya mfuko huo ni
kuagiza na kusambaza vifaa vya michezo hasa kwa watoto wadogo (grassroots) na
vijana.
Mfuko huo utazinduliwa Oktoba 8 mwaka
huu ambayo ni siku ya kilele cha Tanzania kutimiza miaka 50 ya uanachama wake
katika Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “TFF KUANZISHA MFUKO WA MAENDELEO, TENGA NDIYE MWENYEKITI.”
Post a Comment