Friday, May 23, 2014
SASA MAMBO BYEE! MBEYA CITY YAENDA SUDAN
Do you like this story?
Timu ya Mbeya City inaondoka usiku wa kuamkia leo(Mei
22 mwaka huu) kwenda Sudan kushiriki michuano ya Kombe la Nile Basin inayoanza
kutimua vumbi kesho (Mei 23 mwaka huu) jijini Khartoum, Sudan.
Kikosi cha Mbeya City chenye watu 25 wakiwemo
wachezaji 20 kinaondoka saa 2.55 usiku kwa ndege ya Kenya Airways kupitia
Nairobi ambapo kesho (Mei 23 mwaka huu) saa 5 asubuhi kitaunganisha ndege
nyingine hadi Khartoum.
Msafara huo wa kikosi hicho ambao utawasili
Khartoum saa 7.30 mchana kwa saa za huko unatarajia kurejea nyumbani Juni 5
mwaka huu iwapo timu hiyo itafanikiwa hatua ya mwisho ya mashindano hayo.
Michuano ya Nile Basin imeanzishwa mwaka huu na
Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), na
inashirikisha timu zilizoshika nafasi za pili katika ligi za nchi wanachama wa
baraza hilo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “SASA MAMBO BYEE! MBEYA CITY YAENDA SUDAN”
Post a Comment