Monday, May 5, 2014

STARS NA MALAWI ZAINGIZA MIL31 SOKOINE MBEYA.




MPAMBANO wa kirafiki wa kimataifa kati ya Timu ya soka ya Tanzania (Taifa Stars) na Malawi (The Flames) uliochezwa juzi Jijini hapa, umeingiza kiasi cha shilingi milioni 31, 200,000.

Akizungumza na waandishi wa habari,Mwakilishi wa shirikisho la soka nchini (TFF) kwa mikoa ya nyanda za juu kusini, Ayoub Nyenza, amesema kuwa kiasi hicho cha fedha kimetokana na watazamaji 6,240.
Amesema kuwa katika mgao huo, shirikisho la soka nchini TFF na lile la Afrka (CAF) zilipata kiasi cha shilingi milioni 15,236,440, wakati  gharama za tiketi ni shilingi milioni 3,000,000.

Akifafanua zaidi amesema, kiasi cha shilingi  cha sh. milioni 4,759,322 kilichukuliwa na Mamlaka ya mapato nchini (TRA) kama kodi ya ongezeko la dhamani (VAT).

Aidha, Nyenza amesema katika mchanganuo huo, gharama za mchezo zimechukua kiasi cha shilingi milioni 4,668,135, huku wamiliki wa uwanja Chama cha Mapinduzi (CCM) wakiambulia shilingi milioni 3,516,101.

0 Responses to “ STARS NA MALAWI ZAINGIZA MIL31 SOKOINE MBEYA.”

Post a Comment

More to Read