Friday, June 20, 2014
MBASHA ADHAMINIWA UPELELEZI KESI TAYARI
Do you like this story?
MUME wa Flora Mbasha,
Emmanuel Mbasha (32) anayekabiliwa na kesi ya ubakaji amepewa dhamana katika
Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Dar baada ya kutimiza masharti.
Mbasha amefikishwa
mahakamani hapo akitokea Gereza la Keko alikopelekwa Juni 17 mwaka huu
akikabiliwa na kesi ya kumbaka shemeji yake.
Mbasha baada ya
kutolewa kwenye mahabusu ndogo ya mahakamani hapo alionekana mnyonge na
aliyechoka hali iliyosababisha simanzi kwa ndugu na jamaa zake waliokusanyika
mahakamani hapo.
Baada ya kesi hiyo
kutajwa, rafiki wa Mbasha aliyejitambulisha kwa jina la George Mushi na baba wa
mtuhumiwa huyo, Mwahimu Juma walifanikiwa kutimiza masharti ya dhamana.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MBASHA ADHAMINIWA UPELELEZI KESI TAYARI”
Post a Comment