Friday, June 20, 2014
RAIS WA TFF AWAFUNDA MAKOCHA
Do you like this story?
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amewataka makocha wa mpira wa miguu wafanyie kazi
kwa vitendo mafunzo wanayopata badala ya kuweka makabatini maarifa waliyopata.
Akifunga rasmi mafunzo ya wiki mbili
ya makocha wa mpira wa miguu ya Leseni B inayotambuliwa na Shirikisho la Mpira
wa Miguu Afrika (CAF) jijini Dar es Salaam leo (Juni 20 mwaka huu), Rais
Malinzi amewataka makocha hao kuwapa mafunzo ya awali (basic) walimu wa shule
za msingi kwa vile TFF ina mpango wa kuhakikisha kila shule ya msingi nchini
inapata mipira kumi kila mwaka.
“Kila mwaka tutakuwa na mashindano ya
kitaifa ya watoto wenye umri chini ya miaka 13 kuanzia mwaka huu. Hivyo ninyi
makocha huko mnaporudi muwafundishe walimu wa shule za msingi mafunzo ya awali
ya ukocha,” alisema.
Kozi iliyohudhuriwa na makocha 26
kutoka Tanzania Bara na Zanzibar ilikuwa chini ya Wakufunzi wa CAF, Honour
Janza kutoka Zambia, na Sunday Kayuni na Salum Madadi wa Tanzania. Janza pia ni
Mkurugenzi wa Ufundi wa Chama cha Mpira wa Miguu Zambia (FAZ).
Makocha walioshiriki kozi hiyo ni
Abdalla Mohammed Juma (Zanzibar), Abdul Banyai (Temeke), Abdul Nyumba (Temeke),
Abdulmutik Haji (Zanzibar), Aley Mohammed (Zanzibar), Ali Vuai Shein
(Zanzibar), Dennis Kitambi (Morogoro), Dismas Haonga (Ilala), Emmanuel Massawe
(Shinyanga), Fikiri Elias (Arusha), Fulgence Novatus (Mwanza), Hababuu Ali Omar
(Zanzibar), Juma Mgunda (Tanga) na Kidao Wilfred (Ilala).
Wengine ni Maka Mwalwisi (Mbeya),
Malale Hamsini Keya (Zanzibar), Mecky Maxime (Morogoro), Mohammed Tajdin
(Temeke), Mussa Furutuni (Dodoma), Nassor Salum Mohamed (Zanzibar), Peter Mhina
(Ruvuma), Said Mohamed Abdulla (Zanzibar), Salim Makame (Zanzibar), Salum Ali
Haji (Zanzibar), Sebastian Nkoma (Ilala) na Wane Mkisi (Dar es Salaam).
-
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “RAIS WA TFF AWAFUNDA MAKOCHA ”
Post a Comment