Friday, June 20, 2014
WABUNGE WAHOJI KUTOFAUTIANA KWA TAARIFA ZA MAPATO YA SEKTA YA MADINI.
Do you like this story?
Baadhi ya wabunge wamelalamikia
kutofautiana kwa taarifa za mapato husani katika sekta ya madini na
kutaka kamati ya madini kukaa pamoja na kamati ya viwanda na biashara
kupitia mikataba yote ya madini na kuishauri serikali kuvunja mikatapa itakayoonekana
haina maslahi kwa taifa.
Wakichangia mjadala wa mwelekeo
wa mpango wa maendeleo pamoja na bajeti ya mwaka 2014/25, baadhi ya
wabunge bila ya kujali itikadi za vyama vyao wamelalamikia takwimu za
mapato katika sekta ya madini kutokuwa za kweli.
Katika mkutano huo wa kumi na tano
kikao cha thelathimni na sita wamesema kitendo vya wizara mablimbali
kutofuata sheria na kukosekana kwa miiko ya uongozi kumechangia
ongezeko la rushwa na ufisadi na kuwa janga kubwa katika taifa na
kushangazwa na taarifa za mapango wa maendeleo wa taifa kutogusia tatizo la
rushwa jambo linaloweza kusababisha mpango huo kutotekelezeka
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “WABUNGE WAHOJI KUTOFAUTIANA KWA TAARIFA ZA MAPATO YA SEKTA YA MADINI.”
Post a Comment