Friday, June 20, 2014
ALIYEKUWA NA SAKATA LA NYOKA AINA YA CHATU JIJIINI ARUSHA,AWEKA MAMBO HADHARANI
Do you like this story?
Pichani ni Bw.Joseph Magessa aliyetuhumiwa hivi karibuni na tukio la Nyoka aina ya Chatu. |
SAKATA la
kukutwa na chatu eneo la sakina katika nyumba ya Joseph Magessa
limechukua sura mpya baada ya mhusika kuhojiwa na mtandao wa
jamiiblog huu kuhusiana na tukio hilo.
Aidha chatu
huyo ambaye alikutwa nyumbani kwa mmiliki huyo hivi karibuni
imeelezwa tuhuma hizo sio za kweli bali ni njama za kumuharibia tu na tukio
hilo ni la kutengenezwa na watu kwa lengo la kumchafulia jina lake.
Magessa
alisema kuwa ,ameshangazwa sana na tukio hilo kwani lilipotokea alikuwa
safarini yeye na mke wake , ndipo alipopigiwa simu kuhusiana na tukio hilo na
kuwataarifu huyo chatu auawe.
.
Pia, amedai kuwa hizo zinaweza kuwa njama za watu zilizolenga kumchafua na kwamba, suala hilo amemwachia Mungu kwani ndiye ajuaye ukweli.
Pia, amedai kuwa hizo zinaweza kuwa njama za watu zilizolenga kumchafua na kwamba, suala hilo amemwachia Mungu kwani ndiye ajuaye ukweli.
Aliongeza
kuwa, yeye hajawahi kuwa mshirikina wala mke wake bali wanachojua wao ni kuwa
wanamtumikia Mungu na yeye pekee ndiye ajuaye kila jambo na kuwa mambo yote
hayo yaliyotokea amemwachia Mungu ndiye atakayejibu.
Magessa
alifafanua kuwa, ameshangazwa sana na taarifa mbalimbali ambazo zimekuwa
zikizushwa kwenye vyombo vya habari pamoja na mitandao juu ya tukio hilo ila
yeye amenyamaza kimya na amemwachia Mungu kwani ndiye ajuaye kila kitu.
KUHUSU
KUTENGWA KWAKE KANISANI .
Aidha
akizungumzia kuhusiana na swala la kutengwa kwake na Kanisa katoliki alisema
kuwa huo ni uongo na uzushi hakuna kitu kama hicho kwani wanamwelewa vizuri
sana tabia yake na kuwa hana tabia ya ushirikina.
‘Tena waumini
wa kanisa katoliki watakuja kufanya jumuiya nyumbani kwangu na tayari kuna
masalaba pale kama kweli ningekuwa nimefanya hivyo leo hii wangefuata nini hapa
kanisani’alisema Magessa.
Naye mkewe
Selina Magessa , akizungumza na jamiiblog kuhusiana na tukio hilo alisema
kuwa.tangu ameanza kuishi na mumewe miaka mingi hadi sasa hivi ,hajawahi
kusikia wala kuona
vitendo vya
ushirikina.
“Niko na mume wangu miaka mingi, sijawahi kusikia kuwa anafuga nyoka ndani wala sijafiwa na mtoto yeyote, wote watatu wapo ila nashangaa kusikia kauli kwamba mume wangu aliagiza nyoka asiuawe kwa kuwa ni mtoto wake ama mama yake mzazi,” alisema Selina.
Alisema kuwa , kwa sasa hivi ni muda wao kupumzika na kutafakari mambo yao sio wakati wa kuzungumzia swala hilo tena kwani wamechishwa na maneno kila mahali ili wanachofanya ni kumwachia mungu pekee ndiye ajuaye.
Hata hivyo
,Magessa anapenda kuwaelezea watanzania kwamba huyo chatu sio wa kweli ni wa
kurushwa kwenye fensi yake ili amchafulie kwani chatu wa ukweli
asingeweza kuburuzwa hadi kanisani kwani kila mtu anamwelewa mnyama huyo jinsi
alivyo mkali ,kwa hiyo hizo ni njama tu za kuharibiana kwenye maisha .
Hata hivyo Mchungaji huyo alisisitiza kuwa ni vema watanzania wakaelewa na kufahamu kwamba chatu wa ukweli
wanafahamika.
ATOA RAI KWA
VYOMBO VYA HABARI.
Aidha
alivitaka vyombo hivyo kuelimisha jamii badala ya kupotosha ukweli wa jambo
kama ambavyo sakata hilo limezua sura tofauti kwa watanzania .
‘mnajua nyie
ndio vyombo tunavyovitegemea kwa jamii ,sasa mkiandika vitu ambavyo hamna
uhakika navyo mnategemea italeta picha gani kwa jamii ya watanzania ‘alisema
Magessa.(CHANZO Pamela Mollel jamiiblog)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ALIYEKUWA NA SAKATA LA NYOKA AINA YA CHATU JIJIINI ARUSHA,AWEKA MAMBO HADHARANI ”
Post a Comment