Sunday, August 3, 2014

KUHUSU DALADALA KURUHUSIWA KWENDA FERI BADO KITENDAWILI JIJINI DAR.




USAFIRI wa daladala za kwenda Kivukoni uliotarajiwa kuanza mwishoni mwa Julai, umeshindikana kutokana na barabara kutokamilika.

Siku chache zilizopita Mamlaka  ya Usafirishaji wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra), ilitangaza  kurejesha safari hizo bila mafanikio hadi sasa.

Akizungumza kwa njia ya simu, Ofisa Mfawidhi wa Sumatra Kanda ya Mashariki, Conrad Shio alisema daladala zilizositishwa kupita njia hiyo zitaanza pindi barabara zitakapomalizika.

Mamlaka hiyo ilisitisha safari za daladala Septemba 30 mwaka jana na kusababisha malalamiko kutoka wamiliki wa daladala hizo baada ya kuruhusu mabasi ya Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA) kuwa wasafirishaji wa abiri apekee katika njia hiyo.

0 Responses to “KUHUSU DALADALA KURUHUSIWA KWENDA FERI BADO KITENDAWILI JIJINI DAR.”

Post a Comment

More to Read