Thursday, August 14, 2014
MAITI YA KIKONGWE WA MIAKA 62 YAKUTWA KWENYE MFUKO WA KUSAFIRIA NDANI YA BUTI YA TAX.
Do you like this story?
Polisi wa
kisiwa cha Bali nchini Indonesia wanawashikilia watu wawili baada ya mwili wa
mwanamke wa kimarekani kuonekana kwenye mfuko wa kusafiria.
Binti wa
mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 19 pamoja na mpenzi wake mwenye miaka 21
wameshikiliwa na polisi katika hoteli iliyopo ufukweni siku ya Jumatano.
Marehemu
mwenye umri wa miaka 62 Sheila Wiese Mack, alipatikana katika buti ya taksi
akiwa ndani ya mfuko wa kusafiria katika hoteli.
Afisa wa
Indonesia amesema marehemu huyo ameonekana kuwa na majeraha katika uso na
kichwani mwake.
Kulikuwa na ishara ya mahangaiko kwa muathirika
huyo kutokana na kuwa na michubuko katika mikono na vidole vyake vikiwa
vimevunjwa
shirika la
habari la reuters lilimnukuu Afisa Ida Bagus Putu Alit, akisema
Polisi
waliwakamata wapenzi hao baada ya kuwakuta katika hoteli tofauti huko Bali.
Mkuu wa polisi
katika mji mkuu wa Bali wa Denspasar, Djoko Hari Utomo, amewaambia waandishi wa
habari kuwa wapenzi hao ambao ni watuhumiwa walikodi teksi na kuweka mfuko wa
kusafiria kwenye buti.
Dereva wa
teksi hiyo alisema walimwambia wanakwenda kuangalia hoteli lakini watarudi.
Ripoti inasema
dereva wa teksi alishuku mfuko huo ambao ulikuwa na damu ndani yake, na
kuwaomba polisi kuufungua.
Mkuu wa polisi
alisema baada ya mwili kugundulika, polisi waliwapata wapenzi hao wakiishi
katika hoteli nyingine huko Bali.
Polisi
walisema uchunguzi wa mwili wa Bibi Von Wiese-Mack unaendelea.
Taarifa ya
ubalozi wa Marekani nchini Indonesia inasema ubalozi huo umepata taarifa za
kifo cha raia wa Marekani na kwamba watu wawili wamekamatwa kuhusiana na tukio
hilo.
Mama na binti
yake wameripotiwa kuwa wanaishi Chicago, Marekani.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ MAITI YA KIKONGWE WA MIAKA 62 YAKUTWA KWENYE MFUKO WA KUSAFIRIA NDANI YA BUTI YA TAX.”
Post a Comment