Wednesday, August 27, 2014
WATU 7 WATIWA MBARONI KWA TUHUMA ZA KUPORA NA KUUA WANAWAKE JIJINI ARUSHA
Do you like this story?
Watu saba wamekamatwa Jijini
Arusha kwa tuhuma za kuhusika kwenye mauaji ya unyang’anyi wa kutumia
silaha kwa wanawake.
Wanadaiwa pia kusababisha
kifo cha mtoto, Christen Nickos mwenye umri wa miaka mitatu na nusu
mkazi wa Olasiti hapa.
Akizungumza na waandishi wa habari
ofisini kwake, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alisema
watu wawili kati ya saba ambao ni Japhet Lomnyaki (25) mkazi wa Sakina na
Nehemia Kweka (34) mkazi wa Ngaramtoni walifikishwa mahakamani juzi.
Alitaja wengine, Adam Mussa (30) mkazi
wa Majengo, Tito Loomoni (25) mkazi wa Shamsi, Joseph Loomoni (29) mkazi wa
Shamsi, Abdallah Maglan (22) mkazi wa Oldadai na Emmanuel Maglan
(23) wa Oldadai wanaendelea kuhojiwa na polisi.
Alisema wanatuhumiwa kuhusika kwenye
tukio la Agosti 21 mwaka huu maeneo ya Olasiti ambako wakiwa na pikipiki aina
ya Toyo, walimjeruhi kwa kumpiga risasi mtoto Christen sehemu ya mdomo na
kusababisha kifo chake.
Wanatuhumiwa pia kuhusika kwenye tukio
lingine la mauaji ya mwanamke Shamimu Yulu (30) maeneo ya Sakina kwa Idd
ambaye alipigwa risasi na kufariki dunia akiwa anapatiwa matibabu hospitali ya
Selian.
Mwanamke mwingine Flora Porokwa
alilazwa Hospitali ya Arusha Lutheran Medical Centre (Selian) baada ya kupigwa
risasi ya bega kwenye tukio lingine tofauti likihusisha watu waliokuwa kwenye
pikipiki.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ WATU 7 WATIWA MBARONI KWA TUHUMA ZA KUPORA NA KUUA WANAWAKE JIJINI ARUSHA ”
Post a Comment