Wednesday, August 27, 2014
BAADA YA EBOLA KUUA WATU KONGO DRC, MKUU WA MKOA WA KIGOMA AAGIZA HAYA HAPA.
Do you like this story?
Taarifa zinaarifu kwamba kati ya
Wagonjwa nane waliokutwa na Ebola huko Congo DRC, wawili kati yao wamefariki
dunia.
Taarifa hizi zimeendelea kuwashtua na
kuwafanya majirani kuzingatia tahadhari ambapo mkuu wa mkoa wa Kigoma Issa
Machibya amesema:
"Pamoja na tishio la ugonjwa huu kwamba uko DRC Congo (DRC ya mbali sana kule kaskazini wanakopakana na Afrika ya kati na Sudan), tumeanza kuchukua tahadhari kwenye mipaka yetu manake binadamu wanatembea na maingiliano ni makubwa.
‘Kuanzia leo nimemuagiza katibu tawala
wa mkoa magari yote yenye uwezo wa kubeba vipaza sauti usiku au jioni watu
wamesharudi nyumbani yapite kutangazia Wananchi kwa muda wa siku tatu mfululizo
licha ya kuweka vipeperushi"
John Ndunguru ambae ni katibu tawala wa
mkoa amesema" "Kwenye hospitali zetu wameshatenga chumba maalum
kama atatokea mgonjwa yeyote manake inabidi Wagonjwa hawa wawekewe kinga au
wigo kwa siku 48, vilevile wizara ya Afya imeahidi kutuletea vifaa vya kutosha
hasa vya kinga na dawa mbalimbali, tayari maafisa Afya wako hata uwanja wa
ndege kukagua kila anaeingia"
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “BAADA YA EBOLA KUUA WATU KONGO DRC, MKUU WA MKOA WA KIGOMA AAGIZA HAYA HAPA.”
Post a Comment