Saturday, September 6, 2014
KIJANA ALIYEZUA HOFU KUTOKANA NA KUWA NA DALILI ZA EBOLA MTWARA, MAJIBU YAKE YAWEKWA WAZI.
Do you like this story?
KIJANA Ally Selemeni
(30), mkazi wa Mikindani, mkoani Mtwara aliyeleta hofu kwa wananchi waliokuwepo
katika maeneo ya hospitali ya Rufaa ya Ligula kuwa ana dalili za ugonjwa wa
Ebola, anaendelea vema na imebainika hana ugonjwa huo.
Akizungumza na
waandishi wa habari katika hospitali hiyo, Selemani alisema kuwa alilazwa
kutokana na kusumbuliwa na kifua kwa miezi miwili sasa.
Selemani aliyasema
hayo kutokana na uvumi uliojitokeza mkoani humo kwamba ameathiriwa na ugonjwa
wa ebola baada ya kutokwa na damu katika mwili wake kupitia puani na mdomoni
kitendo kilichofanya wauguzi kumkimbia na kwenda kutafuta vifaa vya kujikinga
na gonjwa huo.
“Watanzania wenzangu
naomba wajue kuwa mimi sina ugonjwa wa ebola ila ni maneno ya watu tu baada ya
kuona natoka damu katika mwili wangu wakajua nina huo ugonjwa,” alisema
Naye mdogo wa mgonjwa
huyo, Sanjamin Abdallah (20) alisema kuwa kaka yake anasumbuliwa na kifua na
sio kwamba ameathiriwa na ugonjwa wa ebola kama ilivyoelezwa na baadhi ya watu
waliomuona.
Naye muuguzi
aliyekuwepo zamu siku ya tukio, Mariam Mkanyama, alisema kuwa walipoona mgonjwa
huyo anatokwa na damu puani na mdomoni walishitushwa na hali hiyo.
“Yaani tulipoona
mgonjwa wa kifua anatoka damu puani na mdomoni tulipata na mshtuko mkubwa na
tulikimbia kwenda kuchukua vifaa vya kujikinga zaidi kwa ajili ya kuchukua
tahadhari ya ugonjwa huo,” alisema.
Alisema kuwa tukio
hilo lilitokea Agosti 27 mwaka huu saa 4 asubuhi ikiwa ni siku ya tisa tangu
mgonjwa huyu alazwe hospitalini hapo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “KIJANA ALIYEZUA HOFU KUTOKANA NA KUWA NA DALILI ZA EBOLA MTWARA, MAJIBU YAKE YAWEKWA WAZI.”
Post a Comment