Saturday, September 6, 2014
MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2014 IWAWA SEKONDARI WILAYANI MAKETE, MKUU WA WILAYA ATOA WOSIA
Do you like this story?
Walimu na wanafunzi
wa shule ya sekondari Iwawa iliyopo Makete mkoani Njombe wametakiwa kutoridhika
na kubweteka na shule hiyo kushika nafasi ya nne kitaifa katika matokeo ya
kidato cha sita 2014 yaliyotangazwa miezi michache iliyopita
Kauli hiyo imetolewa
na mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro katika hafla ya kuwapongeza
walimu wa Iwawa sekondari baada ya shule hiyo kushika nafasi ya 4 kitaifa,
nafasi ya 2 kikanda na nafasi ya 1 kwa mkoa wa Njombe katika matokeo ya kidato
cha sita mwaka huu
Amewapongeza walimu
kwa jitihada zao za kufundisha pamoja na moyo wa wanafunzi katika kujisomea
ambavyo kwa pamoja vimepelekea kuitangaza wilaya ya Makete kielimu na kuwataka
kupanda na kushika nafasi za juu katika mitihani inayofuata
"Ni kweli
mnastahili pongezi lakini nawaombeni ongezeni bidii ili mitihani inayokuja
mwakani mpande zaidi ya hapa, muitangaze wilaya yetu, tukishirikina pamoja
tunaweza" amesema Matiro
Katika hatua nyingine
mkuu huyo wa wilaya amewataka wananchi kushirikiana katika kuchangia maendeleo
ya shule kwani serikali inaunga mkono jitihada zao pale tu inapoona wamechangia
Amesema kumekuwa na
kasumba ya watu wachache kuwakatisha tamaa wananchi wengi wenye moyo
wakuchangia miradi ya shule, na kusema wananchi wasikatishwe tamaa na watu wa
aina hiyo kwani serikali haiwaachii peke yao, wao wakichangia kwa kiasi fulani
serikali nayo humalizia palipobakia huku akisisitiza kuwa kwa shule zenye
upungufu wa walimu, serikali inalitambua tatizo hilo na ndiyo maana inapanga
walimu wapya kila mwaka katika shule hizo na mwishowe upungufu huo utamalizika
Awali akisoma taarifa
ya shule kwa mkuu wa wilaya, mkuu wa shule hiyo Mwl. Antony Ng'wavi amesema
shule yake inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo upungufu wa vyumba vya
madarasa pamoja na walimu jambo ambalo linachangia kupungua kasi ya ufaulu kwa
kiasi kikubwa zaidi, huku akiahidi kuwa mwakani shule yake itafanya vizuri
kuliko mwaka huu
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2014 IWAWA SEKONDARI WILAYANI MAKETE, MKUU WA WILAYA ATOA WOSIA ”
Post a Comment