Saturday, September 6, 2014
KUNDI LA AL SHABAAB WAPATA PIGO.
Do you like this story?
![]() |
Taarifa kutoka idara ya ulinzi ya Marekani Pentagon zinasema kuwa mmoja wa wanzilishi wa kundi la Al Shabaab Ahmed Godane ameuawa. |
Marekani imesema kuwa kuuawa kwa Godane ni hatua kubwa sana
katika harakati dhidi ya wapiganaji hao wamekuwa msumari mkali kwa mataifa ya
kanda ya Afrika Mashariki na hata kwa serikali ya Somalia yenyewe.
Katibu wa Pentagon Nchini Rear Admiral John Kirby ametangaza
kuwa Ahmed Godane ameuawa katika oparesheni iliyofanywa nchini Somalia Jumatatu
wiki hii.
Kwa Mujibu wa Admiral Kirby, kuuawa kwa Godane ni pigo kubwa
zaidi kwa kundi hilo la Al shabaab na itasaidia kukabiliana na ugaidi
unaofanywa na kundi hilo eneo la Afrika Mashariki.
Marekani imekuwa ikishirikiana na washirika wake wakuu kukabili
wapiganaji hao wa AL shabaab ambapo katika miaka ya hivi karibuni wamezidisha
mashambulio sio tu nchini Somalia bali hadi nchi jirani.
Wiki iliyopita Kikosi cha kulinda amani chini ya mwavuli wa
Muungano wa Afrika AMISOM kikishirikiana na majeshi ya serikali ya Somalia
kilianzisha oparesheni kali kuwasaka wapiganaji hao wa AL shabaab. Na kufikia
mwanzoni mwa wiki hii Marekani ikajiunga katika oparesheni hiyo ambapo
walishambulia msafara ambao Ahmed Godane alishukiwa kuwa ndani.
Walioshuhudia waliambia BBC kuwa muda mfupi baada ya msafara huo
kushambuliwa, ndege za kivita za helikopta zinazoaminiwa kuwa za Marekani zilishuka
na kubeba maiti zote zilizo kuwepo. Kwa hiyo kwa muda hakukuwa na thibitisho
lolote iwapo Godane mwenyewe aliuawa au la.
Upande wa AL shabaab nao walianza kukusanya watu katika kijiji
karibu na eneo hilo la Shebeele ambako shambulio lilifanywa na kuwaua au
kuwateka wengijne ambao hadi sasa hawajulikani waliko.
AL shabaab hawakuzungumzia iwapo Godane alikuwa miongoni mwa
waliouawa.
Leo asubuhi kulikuwa na picha zilizo sambazwa katika mtandao
ambazo hazikuthibitishwa zilizodai kuwa ni Ahmed Godane bado alikuwa hai.
Al shabaab hawajasema lolote baada ya tangazo la Pentagon
kuthibitisha kifo cha Godane
CHANZO:BBC SWAHILI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “KUNDI LA AL SHABAAB WAPATA PIGO.”
Post a Comment