Friday, September 26, 2014
MAHAKAMA YATOA HUKUMU KESI YA KUBENEA KUHUSU BUNGE MAALUMU LA KATIBA
Do you like this story?
Mahakama Kuu ya
Tanzania iliyokaa chini ya Majaji Augustine Mwarija, Aloysius Mujulizi na Dr
Fauz Twaib imetoa uamuzi wake kufuatia maombi ya Saed Kubenea kama ifuatavyo;
1.Kuna mgongano
mkubwa kati ya toleo la Kiswahili na Toleo la Kiingereza la kifungu cha 25 (2)
cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba.
2. Kwamba pamoja na
mgongano huo, Sheria imekusudia kwamba Madaraka ya Bunge Maalum la Katiba
yatatekelezwa kupitia Rasimu ya Tume ya Mabadiliko ya katiba kama
ilivyowasilishwa kwake.
3. Kwamba mamlaka ya
Bunge Maalumu la Katiba yana mipaka, na kwamba madaraka yake yanaongozwa na
kutekelezwa kupitia Rasimu. Bunge Maalumu la Katiba linaweza kubadili na
kuboresha mapendekezo yaliyomo katika Rasimu mradi tu maboresho yasiende
kinyume na misingi iliyowekwa na kifungu cha 9 (2) cha Sheria ya Mabadiliko ya
katiba, kama ilivyokuwa pia kwa Tume.
4.Mahakama Kuu haina Mamlaka ya kuamua ni kiwango gani Bunge maalumu la Katiba linaweza kuboresha Rasimu kwani hilo ni suala la kisiasa, ingawa Bunge Maalumu la Katiba linafungwa na kifungu cha 9 (2) cha Sheria ya Mabadiliko ya katiba.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MAHAKAMA YATOA HUKUMU KESI YA KUBENEA KUHUSU BUNGE MAALUMU LA KATIBA ”
Post a Comment