Saturday, September 27, 2014
SALALIZYA WAIBUKA NA USHINDI SERENGETI FIESTA SOCCER BONANZA............NISHEEDAH
Do you like this story?
Wachezaji wa Timu ya Mpira ya Salalizya fc kutoka Mabatini wakiwa katika picha yapamoja mara baada ya kuchukuwa ushindi |
Kikosi cha Timu ya Wanafunzi wa TIA wakiwa katika pozi |
Wachezaji wa timu ya baa ya Tugelepo ya Mbata wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya mechi |
Mmoja wa Waandaaji wa Serengeti Fiesta 2014 Ibrahim Masoud akizungumza na mashabiki wa mpira wa miguu waliojitokeza kushuhudia Serengeti super bonanza |
Mratibu wa mashindano ya Soccar Bonanza Bw ibrahim Masoud Akiwa na Mgeni rasmi Bw Patrick Zambi Akikabidhi Zawadi kwa Mshindi wa kwanza ambaye alipata boksi 8 za Bia ya Serengeti. |
Serengeti fiesta...........Sambaza upendo. |
TIMU ya Mpira wa
Miguu kutoka Baa ya Salalizya iliyopo Mabatini jijini Mbeya imeibuka kidedea
katika Bonanza lililoshirikisha Timu za Mabaa lililoandaliwa na Serengeti
fiesta maarufu kwa jina la Serengeti Soccer Bonanza.
Katika Bonanza hilo
lililozishirikisha Timu nne lilifanyika jana katika viwanja vya Chuo cha
Uhasibu Mbeya(TIA) zikiwmo timu kutoka Baa ya Kalembo ya Sokomatola, Tugelepo
ya Mbata na wenyeji Wanafunzi wa TIA.
Timu ya Salalizya fc
ya Mabatini ilijinyakulia zawadi ya Katoni 8 za Bia aina ya Serengeti baada ya
kuishinda timu ya Wanafunzi wa TIA katika fainali kwa magoli mawili kwa nunge
hivyo TIA kuibuka mshindi wa pili na kujinyakulia Katoni 4 za bia.
Awali timu ya
Salalizya iliifunga Tugelepo goli moja kwa bila katika mchezo wa utangulizi na
kasha timu ya TIA kuitoa timu ya Kalembo kwa mikwaju 9 kwa 8 baada ya muda wa
kawaida kutofungana.
Mshindi wa tatu
ilikuwa ni timu kutoka baa ya Kalembo baada ya kuifunga timu ya Tugelepo kwa
mikwaju 4 kwa 2 ya penati katika kumtafuta mshindi wa tatu kutokana na
kutoshana nguvu katika muda wa kawaida.
Hivyo Mshindi wa tatu
alijipatia Katoni Mbili huku timu ya Tugeleo ikijipatia Katoni Moja kutokana na
kuwa mshindi wa nne na wa mwisho.
Katika Bonanza hilo
Mgeni rasmi aliyegawa zawadi kwa washindi alikuwa ni Mkurugenzi wa Hoteli ya
Kimataifa ya PADZ iliyopo Forest Mpya, Patrick Zambi, ambaye alitoa wito kwa
vijana kupenda michezo na kujikita katika mazoezi ili kuimarisha afya zao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “SALALIZYA WAIBUKA NA USHINDI SERENGETI FIESTA SOCCER BONANZA............NISHEEDAH”
Post a Comment