Friday, September 26, 2014
WAFUASI WA BOKO HARAM WAJISALIMISHA.
Do you like this story?
Jeshi nchini Nigeria
limesema zaidi ya wafuasi 260 wa Boko Haram wamejisalimisha Kaskazini mwa nchi
hiyo.
Jeshi hilo limesema
katika mapambano limemuua mtu mmoja ambaye huwa anaonekana kwenye picha za
video za propaganda za Boko haram akijidai kuwa Kiongozi wa wa kundi hilo,
Abubakar Shekau.
Jeshi lilisema kuwa
wapiganaji 135 walijisalimisha wakiwa na silaha zao katika eneo la Biu , jimbo
la Borno siku ya Jumanne. Liliongeza kuwa wengine 133 walijisalimisha Kaskazini
Mashariki mwa Nigeria.
Hata hivyo mwandishi
wa BBC mjini Lagos Will Ross anasema kuwa ni vigumu kuthibitisha madai hayo ya
jeshi.
Mwaka jana jeshi
lilisema kuwa Shekau huenda aliuawa, lakini halikutoa thibitisho lolote.
Hata hivyo ikiwa ni
kweli kuwa wapiganaji hao wamejisalisha basi huenda ni ushindi kwa jeshi la
Nigeria katika vita vyake dhidi ya Boko Haram.
Mwandishi wa BBC nchini
Nigeria amesema kuwa majuma ya hivi karibuni Boko Haram imeshindwa kwa kiasi
kikubwa wakati walipokuwa wakipambana kudhibiti eneo karibu na mji wa Maiduguri
ambalo ni ngome yake.
Jeshi limesema
wafuasi 135 wa Boko Haram wamejisalimisha wakiwa na silaha zao katika majimbo
ya Biu na Borno,halikadhalika wafuasi wengine 133 wanahojiwa.
Kwingineko , Rais wa
Nigeria,Goodluck Jonathan amesema kuwa zaidi ya watu 13,000 waliuawa katika
miaka mitano ya kwanza ya harakati za Boko Haram nchini humo.
Rais Jonathan alisema
hayo katika hotuba yake katika baraza la usalama la Umoja wa Mataifa mjini New
York siku ya Jumatano.
Rais Jonathan pia
alisisitiza kuwa juhudi zinafanywa kuwaokoa wasichana wa Chibok.
bbc
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “WAFUASI WA BOKO HARAM WAJISALIMISHA.”
Post a Comment