Friday, September 26, 2014
MASHEIKH NA MAPADRE KUSAKATA KABUMBU UWANJA WA TAIFA OCTOBA 12 2014.
Do you like this story?
OKTOBA 12 mwaka huu katika kuadhimisha
siku ya amani duniani viongozi wa dini wanatarajia kujitupa katika Uwanja wa
Taifa jijini Dar es Salaam, wakiwa na lengo la kudumisha amani iliyopo nchini.
Mtanange huo utawajumisha
Masheikh,Maimamu,Maaskofu,Wachungaji na Mapadre na mgeni rasmi katika mchezo
anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ambaye tayari amekubali kuungana na
viongozi hao wa dini.
Akizungumza jana jijini, Sheikh
wa Mkoa wa Dar es Salaam ambaye ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya
mchezo huo alisema kuwa Mkuu wa Mkoa huo, Said Sadick atakuwa mwamuzi msaidizi
akisaidiwa na Kamishna wa Kanda Maalumu, Seleman Kova na Afande IGP Ernest
Mangu atakuwa mpuliza kipyenga wa kati.
Alifafanua kuwa viongozi hao wa
dini tayari wameshaanza mazoezi kwa jili ya kujiweka tayari kwa ajili ya
kufanya vizuri katika mtangane huo wa kuhamasisha amani na ulivu nchini katika
uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam.
Aliongeza kuwa wanaendelea na
mazoezi hayo chini ya kocha mjerumani na Serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam,
itazipeleka timu mbili mkoani Morogoro kwa ajili ya kujifua zaidi na mtanage
huo utakaokuwa wa kukata na shoka kutokana na jinsi timu za viongozi hao wa
dini zilivyojipanga kucheza mchezo huo wa amani.
Ili kujindaa vema na mchezo huo
Mwakilishi Mkazi wa Shirilka la KAS,Tanzania, Stefan Reith, jana alikabidhi
Sheikh kwa Dar es Salaam, Alhad Salum vifaa mbalimbali vya michezo ikiwemo
mipira, jeszi na viatu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MASHEIKH NA MAPADRE KUSAKATA KABUMBU UWANJA WA TAIFA OCTOBA 12 2014. ”
Post a Comment