Sunday, October 26, 2014
FISI AFUNGA MITAA MJINI SINGIDA, WANANCHI WATIMUA MBIO NA KUTELEKEZA NYUMBA ZAO.
Do you like this story?
Katika hali isiyo ya
kawaida wakazi wa manispaa ya Singida wameingiwa na taharuki na kuanza kukimbia
ovyo baada fisi kuonekakana katikati ya mji wa Singida akiwa anakimbia na
kuingia katika maduka ya wafanya biashara.
Wakieeleza kwa
hisia tofauti baadhi ya wakazi huku wengine wakiwa wamepanda juu ya mapaa
ya nyumba pamoja na watoto wao kwa hofu ya kuumwa,wamesema kuonekana kwa
fisi mjini katikati ni jambo la ajabu kwani wanyama kama hao honekana
vijiji au porini,wengine wamesema labda mnyama huyo amechelewa kurudi vichakani
wakati alipokuwa amekuja kula mabaki ya chakula mjini.
Akielezea tukio hilo
Afisa maliasili mkoa wa Singida Bwana Charles Kidua amesema pamoja na kwamba
wanyama kama fisi wapo katika manispaa ya Singida na pindi wanapo onekana
katika maeneo ambayo siyo ya kawaida ,Basi wananchi watoe taarifa kwa mamlaka
husika kwani wanyama kama haho wana weza kuwa na ugonjwa wa kichaa
,badala ya kujichukulia hatua mkononi ya kuwaua.
Kutokana na umati wa
wananchi kuwa wengi wakati wakimfukuza fisi huyo bila kujali askari waliokuwa
wakituliza fujo huku wakiwa na silaha,wanachi walifanikiwa kuwapokonya askari
fisi baada ya kumtega na kamba huku wakiimba tunataka fisi wetu na kuamua
kumkimbiza mjini huku wakimpiga umbali wa kilomita mbili.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “FISI AFUNGA MITAA MJINI SINGIDA, WANANCHI WATIMUA MBIO NA KUTELEKEZA NYUMBA ZAO.”
Post a Comment