Monday, October 27, 2014
SERIKALI YAPIGA MARUFUKU UKATAJI WA MITI NCHINI HATA KAMA IKIWA MTU AMEPANDA NYUMBANI KWAKE.
Do you like this story?
Serikali imepiga marufuku ukataji
wa miti nchini hata kama ikiwa mtu amepanda nyumbani kwake anatakiwa kuomba
kibali kwajili ya kukata mti huo.
Akizungumza wilayani Siha juzi
,Waziri wa Maliasili na Utalii , Lazaro Nyalandu amesema kwamba Tanzania inawez
a kuwa jangwa baada ya miaka 15 kutokana na uvunaji mbaya wa bidhaa za miti
unaofanyika nchini .
“Tukiendelea kukata miti kma hivi
tutakuwa tunatengeneza janga la kitaifa kwa hiyo kwa sasa naomba niseme rasmi
kuwa hakuna mtu anaruhusiwa kukata miti au mti hata kama ameupanda nyumbani
kwake, ni lazima aombe kibali kwa maafisa wa misitu. Tunatakiwa kushiriki kwa
pamoja katika kutunza mazingira yetu” amesema
Nyalandu alisema kasi ya ukataji
miti nchini imekuwa kuubwa kwa sasa kutokana na kuongezeka kw aidadi ya watu na
kuwa kwa mwaka mmoja pekee hekta 350,000 hukatwa huku kikiwa hakuna jitihada za
kurejesha iliyoondolewa.
“Kwa kaddri siku zinavyozidi
kwenda na watu kuongezeka baada ya miaka kumi misitu itakuwa inavunwa kw azaidi
ya hekta 850,000 nchini kwa mwaka, hii ni hatari kubwa, lazima tufanye jitihada
zaidi kukomesha tatizo hili”.
Aliwaagiza wakuu wa wilaya za
Arusha na kilimanjaro kuunda timu ili kuandaa hadidu za rejea kwa ajili
ya kupatia kikosi kazi ambacho kitaandaas andiko kw ajili ya kuanzisha mfuko
huo.
Mtendaji Mkuu wa wakala wa
misditu (TFS) Juma Mgoo alisema kwamba misitu ilianza kutunzwa mtokea enzi za
wakoloni lakini tatizio kubwa linalotokea kw asasa ni watu wengi kuivamia
kutokana na mahitaji ya nishati na uchomaji wa misitu.
Alisema kwamba kwa msitu wa asili
kawaida huwa na mita 30 za ujazo wakati kwa upande wa misitu ya kuoandwea huwa
wna ujazo wa zaidi ya mira za ujazo 400 hadi 600 kitu ambacho
alishauri umuhimu w akupanda miti zaidi ili iweze kukabiliana na
ongezeko la mahitaji na kuokoa misitu iliyopo.
Waziri Nyalandu alitoa maagizo ya
kuruhusu nguzio za umeme kupita katika msitu wa wilayani Siha ili kufanywa
wananchi waweze kupata nishati ya umeme ili kuokoa matumizi ya kuni kama
nishati na kulinda misitu.
“Umemem ni nishati mbadala badala
ya kuni na mkaa kwa hiyo napenda kuwaeleza kwamba ni bora miti michache ikatwe
ili pupisha nguzi za umeme ili wananchi wakipata nishati hiyo waache kutumia
kuni na kuharibu misitu na kutumia umeme kama nishati mbadala” alisema.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “SERIKALI YAPIGA MARUFUKU UKATAJI WA MITI NCHINI HATA KAMA IKIWA MTU AMEPANDA NYUMBANI KWAKE.”
Post a Comment