Thursday, October 2, 2014
TANZANIA YATAJWA KUWA NA IDADI NDOGO YA WAZEE
Do you like this story?
Tanzania imetajwa kushika nafasi ya 92 katika orodha ya nchi zenye idadi
kubwa ya wazee kati ya nchi 96 duniani huku takwimu za taasisi ya Helpage
International zikionyesha kuwa ifikapo mwaka 2050 idadi ya wazee itakuwa sawa
na ya watoto.
Akiongea jijini Dar es salaam wakati Tanzania imejumuika na nchi nyingine
duniani kuadhimisha siku ya wazee Mkurugenzi wa Taasisi ya Helpage Bi. Amleset
Tewodros amesema Takwimu zinaonesha kuwa katika nchi 96 duniani idadi ya wazee
ambao wanaanzia umri wa miaka 60 imeongezeka hadi kufikia asilimia 91 ya idadi
ya watu duniani huku asilimia 4 tu ya wazee wakipata pensheni ya uzeeni na
asilimia 73 wakiachwa huku wengi wao wakitegemea kilimo kama nyenzo ya uchumi
wao.
Hata hivyo, Tewodros amesema ukuaji wa uchumi pekee hauwezi kuboresha ustawi wa wazee na kuitaka serikali ya Tanzania kuweka sera zenye kusimamia maslahi na yenye kutoa huduma kwa wazee na kushughulikia matokeo ya uzeeni.
Kwa upande wao wazee Juma Mwita na Amani Mbirikira wamesema serikali haijaonesha jitihada kubwa katika kuwasaidia wazee hasa waliopo katika maeneo maalumu yaliyotengwa kwa ajili ya kuwatunza wazee na kueleza ukosefu wa lishe bora unazorotesha afya za wazee nchini.

Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “TANZANIA YATAJWA KUWA NA IDADI NDOGO YA WAZEE ”
Post a Comment