Thursday, October 2, 2014
TAARIFA SAHIHI KUHUSU MWANASHERIA MKUU WA ZANIBAR KUTOLEWA NDANI YA UKUMBI WA BUNGE
Do you like this story?
Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman akisindikizwa kutoka ndani ya ukumbi wa Bunge Maalum jana mjini Dodoma na Askari Polisi. |
Kumekuwa
na Taarifa potofu zinazosambazwa na baadhi ya watu katika mitandao ya kijamii
ya kuwa “Mwanasheria Mkuu Zanzibar Othman Masoud Othman amekamatwa baada ya
kupiga kura ya hapana Bungeni leo”.
Tunapenda
kuutarifu Umma wa Watanzania kuwa, taarifa hizo sio sahihi na ni porojo zenye
kutaka kuleta hisia potofu kwa wananchi kuhusu kiongozi huyo.
Ukweli
wa Jambo hili ni kuwa Mhe. Othman Masoud Othman ametekeleza haki yake ya
Kidemokrasia ya kupigia kura Rasimu ya Katiba inayopendekeza katika Bunge
Maalum . Ambapo katika kura alizopiga, ameweza kuzikubali baadhi Ibara
na kuzikataa ibara nyingine katika rasimu ya Katiba inayopendekezwa.
Pengine
hatua hiyo ya kuzikataa baadhi ya Ibara, haikuwafurahisha baadhi ya Wajumbe na
hivyo kuleta majibishano ndani ya Bunge Maalum wakilalamikia uamuzi wake huo.
Kutokana
na hofu hiyo ya baadhi ya Wajumbe kuanza kupinga uamuzi wake huo ndani ya
Bunge, Ofisi ya Bunge Maalum kama ilivyokawaida kwa kila mjumbe, imeweza
kumpatia Ulinzi Maalum wakati akitoka Bungeni hadi alipoondoka katika viwanja
vya Bunge ili asiweze kubugudhiwa kwa namna yoyote ile kutokana na uamuzi
wake huo.
Suala
hili limechukuliwa kipropaganda na kuanza kueneza uongo katika mitandao ya
kijamii kuwa Mhe. Othman amekamatwa baada ya kupiga kura ya hapana.
Tunapenda
kuwahakikishia Watanzania wote kuwa Mhe. Othman hajakamatwa bali alipewa ulinzi
katika Maeneo ya Bunge Maalum jambo ambalo hufanyika kwa kila mjumbe ambaye kwa
namna moja ama nyingine itaonekana kuna dalili za kubugudhiwa katika Maeneo ya
Bunge kutokana na uamuzi au kitendo alichofanya. Na kutokana na hali ilivyo,
ulinzi wake umeimarishwa pia mahali alipo kwa hivi sasa mpaka atakapomaliza
kazi yake hapa Dodoma.
Kanuni
za Bunge Maalum zimempa madaraka Katibu wa Bunge Maalum kusimamia masuala yote
ya Ulinzi na Usalama kwa Wajumbe na Maeneo yote ya Bunge Maalum.
Imetolewa
na Idara ya Habari
Ofisi
ya Bunge Maalum
Dodoma
1
Oktoba, 2014
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “TAARIFA SAHIHI KUHUSU MWANASHERIA MKUU WA ZANIBAR KUTOLEWA NDANI YA UKUMBI WA BUNGE ”
Post a Comment