Thursday, October 23, 2014
WAZIRI MKUU AZINDUA JARIDA LA FIRST JIJINI LONDON
Do you like this story?
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amezindua jarida la kimataifa
la FIRST ambalo limesheheni taarifa za kuitangaza Tanzania kwa wadau wa nchi
mbalimbali duniani huku likielezea hatua mbalimbali za ustawi kwa miaka 50
tangu nchi ipate uhuru.
Uzindusi huo ulifanyika kwenye ofisi za ubalozi wa
Tanzania jijini London, Uingereza ambako pia Waziri Mkuu alikabidhiwa nakala ya
kwanza ya toleo la sasa ambayo iliwekwa kwenye jalada jekundu la ngozi (leather
bound red cover).
Akizungumza katika uzinduzi huo, Waziri Mkuu alisema
Serikali ya Tanzania imepata fursa nzuri ya kujinadi kwa watu maarufu na
wafanyabiashara wa kimataifa duniani kupitia jarida hilo na akataka uwekwe
utaratibu wa kujinadi kisekta.
Alimtaka Balozi wa Uingereza, Bw. Peter Kallaghe aweke
mkazo na kusimamia suala hilo ili kuhakikisha matoleo yanayofuata yanakuwa ya
kisekta zaidi. “Balozi hapa umefanya kazi nzuri sana ya kuinadi nchi yetu, wala
usichoke. Tujitahidi sasa kila mwaka waandike kuhusu fursa za uwekezaji kwa
miradi ya kisekta kama utalii, nishati, madini na kadhalika,” alisema.
Waziri Mkuu alimshukuru Mwenyekiti wa taasisi ya First,
Bw. Rupert Goodman kwa kazi nzuri aliyoifanya kwa ajili ya Taifa la Tanzania.
“Kazi uliyoifanya ni nzuri lakini katika tolea lijalo tuangalie jinsi ya
kuitangaza miradi ya uwekezaji ambayo inauzika na iende sekta kwa sekta.
Ukisirikiana na Balozo wetu hapa, lazima utapata kitu kizuri,” alisema.
Mapema, akielezea kuhusu jarida hilo la FIRST, Balozi
Kallaghe alisema jarida hilo linasambazwa kwenye mashirika mbalimbali ya ndege
kama vile British Airways, Air Astana, Lufthansa, United Airlines, Gulf Air,
American Airlines, South African Airways, Korean Airways, Etihad Airways, Qatar
Airways na Continental Airlines.
“Siyo tu kwamba linasambazwa katika mashirika haya ya
ndege, bali pia linawekwa kwenye vyumba vya kupumzikia (First Class and
Business Class Lounges) abiria wa daraja la kwanza na la pili wa mashirika haya
kwenye viwanja vingi vya ndege,” alisema.
Alisema hili ni toleo la sita ambalo limeandaliwa kwa
ushirikiano na ofisi yake (Ubalozi wa Uingereza) ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho
ya Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania lakini pia ikilenga kutangaza fursa za
uwekezaji lakini pia ikitangaza hatua mbalimbali za maendeleo ambazo nchi hii
imepitia.
Uzinduzi huo ulihudhuriwa pia na Naibu Waziri wa Fedha,
Bw. Mwigulu Nchemba; Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Bw. Mahadhi Maalim na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Bw. Charles Kitwanga.
Wengine ni Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba na Mkuu wa Mkoa wa
Ruvuma, Bw. Said Mwambungu ambao pia wamefuatana na Waziri Mkuu.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
ALHAMISI, OKTOBA 23, 2014
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “WAZIRI MKUU AZINDUA JARIDA LA FIRST JIJINI LONDON ”
Post a Comment