Thursday, October 23, 2014

KAMPUNI YA JAGRO ENTERPRISESS YAKAMATA GARI YA TAASISI YA KIBENKI NMB TAWI LA MBEYA.



Gari ya Nmb ambayo imekamatwa


Mwana Sheria wa Kampuni ya Jagro Enterprises Bw Aloyce Mrema akitolea maelezo juu ya kukamatwa kwa Gari hilo




Mkurugenzi wa Jagro Enterprisess Bw Maulid Hamis akimtolea ufafanuzi Mwanasheria juu ya ukamatwaji wa Gari hilo la Nmb


Gari ya Kampuni ya Vodacom ikiwa kwenye Eneo la maegesho ya Kampuni ya Jagro mara baada ya kulikamata


MAHAKAMA ya Wilaya ya Chunya, Mkoani Mbeya, imetoa kibali cha kukamatwa na kuuzwa kwa magari matatu  ya Taasisi ya Kibenki ya NMB na  Kampuni ya mawasiliano Vodacom Tanzania, ili kulipa fidia ya shilingi milioni 86,553,700 kwa kosa la kumsababishia mteja hasara baada ya kuhamisha fedha kwenye akaunti kwa kutumia huduma ya  kibenki  ya njia ya simu bila idhini yake.
Kesi hiyo namba 4 imefunguliwa mahakamani hapo, Mei 13 mwaka huu na mlalamikaji Mwanswa Jonas dhidi ya Taasisi ya kibenki ya NMB na kampuni ya Vodacom Tanzania  na mahakama hiyo kutoa hukumu Oktoba 13 mwaka huu kwa kutoa kibali cha kuuzwa kwa magari hayo.
Akisoma shitaka hilo, hivi karibuni, Kalani wa mahakama ya Wilaya ya Chunya Izza Sheumu, mbele ya hakimu wa Wilaya, Desdery Magezi, alisema, Mei 13,2014 , mlalamikaji alibaini kupotea kwa fedha zake zikiwa na thamani ya shilingi milioni 6,553,700 zilizokuwa kwenye akaunti namba 6071600335 kupitia benki ya NMB.
Amesema, uchunguzi ulibaini kuwa fedha hizo zilipotea baada ya kuhamishwa kwa kutumia huduma ya kibenki ya njia ya simu kutoka akaunti namba 6071600335 kwenda kwenye namba ya simu  ya mkononi ya Vodocom 0768 713668 bila ya idhini ya mteja.
Amesema, imeelezwa kuwa wakati zoezi hilo linafanyika mteja huyo alisitishiwa huduma ya mawasiliano kwa muda na kwamba alipofuatilia kwenye ofisi za Vodacom, alielezwa kwamba asubiri huduma yake itarudishwa kwani kunamatatizo ya kiufundi.

0 Responses to “KAMPUNI YA JAGRO ENTERPRISESS YAKAMATA GARI YA TAASISI YA KIBENKI NMB TAWI LA MBEYA.”

Post a Comment

More to Read