Thursday, October 23, 2014
BASATA KUMVUA TAJI LA U-MISS ,MREMBO SITTI MTEMVU ALIYEDANGANYA UMRI WAKE
Do you like this story?
Akizungumza na waandishi wa habari ndani ya Ukumbi wa
Ngorongoro katika Hoteli ya JB Belmont, Posta Mpya jijini Dar es Salaam, Sitti
alisema ana miaka 23 kwa kuwa alizaliwa mwaka 1991.
Pamoja na Lundenga kuweka wazi mchakato waliyotumia hadi
kumfanya Sitti kuibuka na taji la Miss Tanzania 2014, bado kuna dosari za wazi
ambazo zilijionesha kuwa mrembo huyo analazimisha safari hiyo kwani cheti chake
cha kuzaliwa kinaonesha ana miaka 23 lakini namna cheti hicho kilivyotolewa
ndiyo utata na ulazima ulipotokea.
Baadhi ya waandishi walimuhoji Sitti juu ya cheti hicho
ambacho kinaonesha kimetolewa na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Uzamini (RITA),
Septemba 9, mwaka huu, siku 32 tu kabla ya kutwaa taji hilo.
Swali ambalo lilitawala
kwenye kikao hicho lilikuwa ni kwa nini cheti hicho kitoke ndani ya muda mfupi
wakati anaonekana alikuwa akiishi nje ya nchi kwa muda mrefu, na kwamba huwezi
kuishi nje ya nchi bila paspoti ambayo pia upatikanaji wake unatakiwa kuwa na
cheti cha kuzaliwa alisema kilipotea!
Akaulizwa alitoa ripoti kituo gani cha polisi ili waandishi
waende kuulizia, akagoma!
“Mimi nadhani alichoongea Hashim Lundenga kinajitosheleza na
zaidi naona mnanisakamasakama bila sababu ya msingi, nimechoka kuandamwa na
vyombo vya habari pamoja na mitandao.
“Kama kuna mtu anaona cheti hakiko sahihi basi aende ofisi
husika ili ajiridhishe juu ya hilo hata suala la kuniambia nina mtoto nafikiri
mnaweza kwenda hospitali yoyote kuulizia hilo,” alisema Sitti.
..amekaa pembeni ili aweze kumfafanulia japo kwa ufupi juu ya
mkanganyiko huo kama tangu alipomzaa Sitti hakuwahi kumchukulia cheti cha
kuzaliwa hadi alipoamua kushiriki mashindano hayo.
“Mambo ya Sitti naomba muulize yeye maana ndiye mshiriki wa Miss
Tanzania, mimi sijawahi kushiriki hata siku moja na hapa nimekuja kumleta yeye
tu, hivyo siwezi kuzungumza lolote juu ya hilo, kikao hiki kimeandaliwa na Miss
Tanzania na si ukoo wa Mtemvu,” alisema mama huyo.
Hili ni bomu la pili, la kwanza ni lile lwa kudai ana miaka
18 siku alipojitambulisha kwenye shindano hilo, Mlimani City, Dar na kuzua
utata mkubwa kwenye jamii.
Source GPL
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ BASATA KUMVUA TAJI LA U-MISS ,MREMBO SITTI MTEMVU ALIYEDANGANYA UMRI WAKE ”
Post a Comment