Wednesday, October 22, 2014
WAANDHISI WA HABARI WANUSURIKA KUCHEZEA KICHAPO HUKO DODOMA
Do you like this story?
WAANDISHI wa habari
wa mjini Dodoma, wamenusurika kushambuliwa kwa kipigo na Mwenyekiti wa Kijiji
cha Kongogo, Daud Husein baada ya waandishi hao kubaini maonevu na ubabe
anaowatendea wananchi.
Mwenyekiti huyo,
aliwashabulia waandishi kwa matusi na maneno makali huku akiwabeza kuwa ni
makanjanja kwa madai kuwa wasingeandika kero za wananchi bali matendo yake.
Alisema kuwa
waandishi hao walitakiwa kuwapuuza walalamikaji kwa madai kuwa aliwakarimu
waandishi, hivyo hawakuwa na sababu ya kuandika uozo wake. Hali hiyo
ilijitokeza kabla kuanza kwa mkutano wa kijiji cha Kongogo na vijiji vya jirani
ambao lenga lake lilikuwa ni kupinga mradi wa ujenzi wa lambo la kunyweshea
mifugo ambalo wananchi wanalipinga wakidai hawajashirikishwa.
Kwa pamoja wananchi
wa vijiji vya Tinahi, Asanje, Babayu na Kongogo walisema mtendaji wa kijiji cha
Kongogo amekuwa akiwaburuza na kujiamria mambo yake.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “WAANDHISI WA HABARI WANUSURIKA KUCHEZEA KICHAPO HUKO DODOMA ”
Post a Comment