Wednesday, October 22, 2014
BABU TALE ASHIKILIWA NA POLISI KUHUSU DIAMOND KUTINGA MAGWANDA YA JESHI, KAMANDA WA POLISI AZUNGUMZA
Do you like this story?
Kufuatia tukio la
Diamond Platinumz kuonekana akiperform na sare zinazoaminika kuwa za jeshi la
Wananchi (JWTZ), imeelezwa kuwa jeshi la Polisi limemshikilia meneja wa
Diamond, Babu Tale na inaelezwa kuwa alilala selo.
Kwa mujibu wa chanzo
chetu kilichokuwa katika eneo la kituo cha polisi cha Osterbay, Dar es Salaam
jana (October 21), Babu Tale alifikishwa katika kituo hicho ambapo maafisa
kadhaa wa jeshi na polisi walionekana katika eneo hilo.
Chanzo hicho
kimeeleza kuwa Uongozi wa Diamond ulipewa muda wa kujieleza kabla ya saa mbili
asubuhi, October 21 lakini haukufanya hivyo na ndipo hatua hiyo ikachukuliwa.
Haijafahamika bado
kwa nini jeshi la Polisi lilimshikilia Babu Tale peke yake bila Diamond lakini
vyanzo vimeeleza kuwa mwanamuziki huyo yuko safarini.
Hadi habari hii
inaenda hewani, namba ya simu ya Babu Tale ilikuwa haipatikani.
kamanda wa polisi wa
mkoa wa kipolisi wa Kinondoni, Dar es Salaam, Camillus Wambura ambaye amesema
bado hajawasiliana na kituo cha Osterbay kuhusu suala hilo na hajapata taarifa
kwa kuwa kesi hiyo inachunguzwa na iko chini ya mkuu wa upelelezi wa Mkoa.
“Mimi ninachojua kuwa
suala hilo liko chini ya uchunguzi. Habari ya kushikiliwa watu na nini bado sijafahamu.
Najua tu suala hilo liko chini ya uchunguzi na linafanyiwa uchunguzi.
Hiyo ni kesi ambayo iko chini ya mkuu wa upelelezi wa Wilaya, chini ya mkuu wa
upelelezi wa Mkoa. Kwa hiyo sijapokea taarifa ya uchunguzi huo ulipofika.”
Akijibu kuhusu
taarifa za uongozi wa Diamond na Diamond kupewa muda wa kujieleza, Kamanda
Wambura alijibu:
“Uchunguzi unafanywa
huko. Kwa sasa hivi sina taarifa hiyo nina mambo mengi sana. Kwa hiyo kwa sasa
hivi uchunguzi unafanywa chini ya Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa. Kwa hiyo sijapata
nafasi ya kujua wamefikia wapi katika uchunguzi wa suala hilo,”ameongeza
kamanda Wambura.
Mapema wiki hii,
jeshi la wananchi Tanzania lilitoa taarifa kwa vyombo vya habari likipiga
marufuku raia kuvaa sare za jeshi.
chanzo:timesfm
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “BABU TALE ASHIKILIWA NA POLISI KUHUSU DIAMOND KUTINGA MAGWANDA YA JESHI, KAMANDA WA POLISI AZUNGUMZA ”
Post a Comment