Wednesday, October 22, 2014
MAHAKAMA YAAMURU KUKAMATWA KWA MAGARI YA NMB NA VODACOM MBEYA.
Do you like this story?
MAHAKAMA ya Wilaya ya Chunya,
Mkoani Mbeya, imetoa kibali cha kukamatwa na kuuzwa kwa
magari matatu ya Taasisi ya Kibenki ya NMB na Kampuni ya
mawasiliano Vodacom Tanzania, ili kulipa fidia ya shilingi milioni 86,553,700
kwa kosa la kumsababishia mteja hasara baada ya kuhamisha fedha kwenye akaunti
kwa kutumia huduma ya kibenki ya njia ya simu bila idhini
yake.
Kesi hiyo namba 4 imefunguliwa
mahakamani hapo, Mei 13 mwaka huu na mlalamikaji Mwanswa Jonas dhidi ya Taasisi
ya kibenki ya NMB na kampuni ya Vodacom Tanzania na mahakama hiyo kutoa
hukumu Oktoba 13 mwaka huu kwa kutoa kibali cha kuuzwa kwa magari hayo.
Akisoma shitaka hilo, hivi
karibuni, Kalani wa mahakama ya Wilaya ya Chunya Izza Sheumu, mbele ya hakimu
wa Wilaya, Desdery Magezi, alisema, Mei 13,2014 , mlalamikaji alibaini kupotea
kwa fedha zake zikiwa na thamani ya shilingi milioni 6,553,700 zilizokuwa
kwenye akaunti namba 6071600335 kupitia benki ya NMB.
Amesema, uchunguzi ulibaini kuwa
fedha hizo zilipotea baada ya kuhamishwa kwa kutumia huduma ya kibenki ya njia
ya simu kutoka akaunti namba 6071600335 kwenda kwenye namba ya
simu ya mkononi ya Vodocom 0768 713668 bila ya idhini ya mteja.
Amesema, imeelezwa kuwa wakati
zoezi hilo linafanyika mteja huyo alisitishiwa huduma ya mawasiliano kwa muda
na kwamba alipofuatilia kwenye ofisi za Vodacom, alielezwa kwamba asubiri
huduma yake itarudishwa kwani kunamatatizo ya kiufundi.
Amesema,
mlalamikaji huyo akiwa katika harakati za kuweka kiasi cha fedha cha
shilingi milioni 16 kupitia kwenye akaunti yake iliyopo katika benki ya NMB
kabla ya kuweka fedha hizo aliomba salio na kuambia salio lake halitoshi licha
ya akaunti yake kudaiwa kuwa na kiasi cha fedha zaidi ya shilingi
milioni sita.
Amesema, alipofuatilia
alishangazwa kuelezwa kwamba fedha hizo alizitoa yeye kupitia namba yake ya
simu ya mkononi ya Vodocom jambo ambalo alilipinga hivyo kuamua kupeleka
malalamiko yake kwenye ofisi za wanasheria Tanganyika Law Society na kesi hiyo
kusimamiwa na wakili wa kujitegemea, Radlsaus Lwekaza, ambaye aliiomba mahakama
kusikiliza kesi hiyo, Julai 24, mwaka huu.
Pia, imeelezwa kuwa wakili,
Rwekeza, aliiomba mahakama kusikiliza kesi hiyo upande mmoja, kwa kuelezea
kwamba wadaiwa wameamua kwa makusudi kutohudhuria na kujitetea kwenye kesi
husika baada ya mahakama kuhairisha kesi hiyo mara nyingi bila ya wao kutokea
licha ya kupelekewa hati ya kuitwa.
Amesema, baada ya hapo kesi
ilisikilizwa upande mmoja, na mahakama hiyo kutoa hukumu 15/8/2014
ya kwamba mshitakiwa namba moja ambaye ni NMB alipe shilingi milioni 43,
272,750 na Vodacom alipe milioni 43,272,750 ambapo mdai aliomba kukazia hukumu
baada ya siku 30 za rufaa kupita na mahakama ilimkubalia na hatimaye Oktoba 13
mwaka huu mahakama ilitoa kibali kwamba magari mali ya NMB na Vodacom kuuzwa.
Mahakama hiyo, iliyataja magari
hayo kuwa ni gari namba T519 CHP Nissan Patrol nyeupe , T947 CVE Toyota Land
Cruiser mali ya Taasisi ya Kibenki ya NMB na gari namba T388 CGW Nissan Hard
Bord mali ya kampuni ya Vodocom.
Aidha, mahakama hiyo ilitoa
kibali kwa Kampuni ya Jagro Enterprices limited, inayomilikiwa na Maulid Hamis
kukamata magari hayo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MAHAKAMA YAAMURU KUKAMATWA KWA MAGARI YA NMB NA VODACOM MBEYA.”
Post a Comment