Monday, November 3, 2014
AFCON 2015 EBOLA HATMA KUJULIKANA LEO
Do you like this story?
Shirikisho la
soka barani Afrika CAF hii leo linatarajiwa kukaa kikao chake cha mwisho
kitakachofikia maamuzi ya kufanyika ama kutofanyika kwa michuano ya kombe la
mataifa ya Afrika mwaka 2015.
Kikao hicho
kitahusisha uongozi wa CAF , kamati ya maandalizi pamoja na uongozi wa juu wa
serikali ya Morocco kufikia uamuzi wa mwisho wa kusogeza mbele michuano hiyo au
kuruhusu ifanyike kama ilivyopangwa .
Michuano hiyo
iliyopangwa kufanyika mwezi januari mwaka 2015 kama ilivyo kila baada ya miaka
miwili imeingia kwenye hati hati ya kufanyika kufuatia hofu ya ugonjwa wa ebola
ambayo imesababisha wenyeji Morocco kuomba michuano hiyo kuahirishwa .
CAF ilianza
mchakato wa kutafuta mwenyeji mbadala ambapo ilizungumza na mataifa kama Afrika
Kusini , Ghana na Misri kuwaandaa kama Morocco wataendelea na msimamo wao wa
ktuaka michuano hiyo kuahirishwa au kuhamishwa na Ghana pamoja na Misri
wameonyesha dhamira ya kuwa wenyeji .
Afrika Kusini
kwa upande wao wamejitoa kwenye mchakato huo baada ya waziri wa michezo wa
taifa hilo Fikile Mbalula na rais wa chama cha soka SAFA kusema kuwa Afrika
Kusini haitakuwa tayari .
Michuano ya
kombe la mataifa ya Afrika kwa kawaida hufanyika kila baada yua miaka miwili na
mara zote huwa inafanyika mwezi januari lakini kwa michuano ya mwaka 2015 hali
inaweza kuwa tofauti kutokana na hofu ya kusambaa kwa ugonjwa wa ebola ambao
hadi sasa umesababisha vifo vya watu zaidi ya 3000 huku mataifa ya Afrika
Magharibi yakiathirika zaidi .
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “AFCON 2015 EBOLA HATMA KUJULIKANA LEO”
Post a Comment