Monday, November 3, 2014

BARACK NA MICHELLE OBAMA WADAIWA KULUMBANA TENA, KISA MWANAMKE.




Kwa mujibu wa habari zinazoandikwa kwenye mitandao ya nchini Marekani, Michelle Obama anadaiwa kumfukuza mumewe Barack Obama nje ya ikulu ya White House baada ya kudaiwa kumchombeza mwanamke aliyechumbiwa wakati wakipiga kura huko Chicago hivi karibuni
Tukio hilo lililomhusisha msichana aitwaye Aia Cooper, liliandikwa sana na vyombo vya habari kama jambo la utani tu kwakuwa Obama alikuwa akimtania msichana huyo pamoja na mpenzi wake.

Tukio hilo lililomhusisha msichana aitwaye Aia Cooper, liliandikwa sana na vyombo vya habari kama jambo la utani tu kwakuwa Obama alikuwa akimtania msichana huyo pamoja na mpenzi wake.

Katika tukio hilo, mchumba wa Cooper alipita karibu na Rais Obama wakati akiwa kwenye chumba cha kupiga kura ambako Aia alikuwa akipiga yake pia na kumwambia “don’t touch my girlfriend.”

Obama alisikika akisema: There’s an example of a brother just embarrassing me for no reason, just for no reason whatsoever.”

Kwa wengi, jambo hilo liliishia hapo lakini kwa mujibu wa ripoti za hivi karibuni Michelle hakufurahishwa nalo hata kama lilikuwa la utani. Inadaiwa kuwa baada ya Michelle Obama kuona video hiyo alichukia.

Chanzo kimoja kimesema: The way it’s going, Barack may be living elsewhere by the time his second term ends. Michelle’s about to kick him out for good!”

Hii si mara ya kwanza Michelle anadaiwa kuchukia baada ya mumewe kuonesha uchombezaji kwa mwanamke mwingine. Mwaka jana kwenye mazishi ya Mandela, Michelle alidaiwa kuchukizwa na kitendo cha mume wake kuwa karibu mno na waziri mkuu wa Denmark Helle Thorning-Schmidt ambako walipiga selfie pamoja na waziri mkuu wa Uingereza, David Cameron.

0 Responses to “BARACK NA MICHELLE OBAMA WADAIWA KULUMBANA TENA, KISA MWANAMKE.”

Post a Comment

More to Read