Sunday, April 19, 2015
BALOTELLI NDIYE MCHEZAJI ANAYEONGOZA KWA KUBAGULIWA EPL
Do you like this story?
Mshambuliaji wa Liverpool Mario Balotelli. |
Mshambuliaji wa Arsenal Danny Welbeck. |
Takwimu zimeripotiwa
hivi karibuni na Kick it
Out, zinaonesha kuwa Mario Balotelli ndiye mchezaji
aliyebaguliwa sana katika ligi ya Uingereza, huku mchezaji huyo akipokea zaidi
ya ujumbe 8000, asilimia 50 kati ya hizo zikiwa ni za kibaguzi.
Kick it Out wameripoti takwimu hizo za
kushtua, ambao walibaini kwamba raia huyo wa Itali (Mario Balotelli) alilengwa
sana katika mitandao ya Twitter huku mshambuliaji wa Arsenal Danny Welbeck
akipokea ujumbe 1700 asilimia hamsini kati ya hizo zikiwa za kibaguzi.
Mshambuliaji mwenza wa Balotelli katika
kilabu ya Liverpool Daniel Sturridge pia alionekana kulengwa katika mitandao ya
kijamii baada ya kupokea ujumbe wa 1600 asilimia 60 ikiwa ni ujumbe wenye
mwelekeo wa kijinsia.
Utafiti huo pia umebaini kwamba kilabu ya
Chelsea ndio kilabu iliobaguliwa zaidi kwa ujumbe 20,000 huku liverpool ikiwa
ya pili na ujumbe 19,000 Arsenal ikiwa ya tatu kwa ujumbe 12,000 huku
Manchester City na Manchester United zikipokea ujumbe 11,000.
NA BBC
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “BALOTELLI NDIYE MCHEZAJI ANAYEONGOZA KWA KUBAGULIWA EPL”
Post a Comment