Sunday, April 19, 2015

MOTO WATEKETEZA MADUKA MJINI TUNDUMA.




Wananchi wakijaribu kuokoa mali zilizopo katika maduka hayo.Picha na Saimen Mgalula


Kikosi cha Zimamoto kwa kushirikiana na wananchi wa eneo hilo kuuzima moto huo ambao umetekteza maduka zaidi ya Manne katika eneo hilo Mtaa wa Unyamwanga Kisimani mjini Tunduma.
 


Na Mwandishi wetu,Mbeya
MOTO mkubwa umeteketeza maduka zaidi ya Manne    katika mtaa wa Unyamwanga Kisimani Mjini Tunduma  mkoani Mbeya  April 19 mwaka huu.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kudai kuwa moto huo ulitokea saa 2   usiku mtaa wa unyamwanga ambapo maduka hayo yaliyoteketea yalikuwa katika  jengo moja linalomilikiwa Albart Ndembwike mkazi wa Tunduma .
Kamanda Msangi amesema  moto huo ulitokea katika moja ya duka kati ya hayo Manne yaliteketea kwa moto ambapo chanzo chake bado hakijafahamika mara moja ambapo uchunguzi wa tukio bado unaendelea .

Amesema changamoto kubwa iliyopo katika eneo hilo LA Mji wa Tunduma ni ukosefu wa gari la zima moto hivyo katika tukio la jana walilazimika kuomba msaada kwa majirani zao Zambia ambao walifika mara moja na kuuzima moto huo kwa kushirikiana na wananchi wa eneo hilo.

Amesema changamoto hiyo inatokana na wananchi wenyewe kufanya uhalibifu katika gari la zima moto lililokuwepo katika mjini huo ambalo lilihalibiwa vibaya kwa kutupiwa mawe kipindi nyuma ambalo kwa sasa lipo katika matengenezo.

Aidha jeshi la polisi limelaani mtindo unaoota mizizi hivi sasa wa wananchi kujichukulia sheria mkononi kwani kwa kufanya shambulio kwa kikosi cha zima moto mara kinapo wasili katika eneo la tukio.

Amesema mashambulio ya aina hiyo yamekuwa yakisababisha hasara ikiwa ni pamoja na kuvunjwa vioo vya gari, kupotea kwa vitendea kazi pamoja na baadhi ya askari wa zimamoto kujeruhiwa kitendo ambacho kinavunja moyo kwa askari hao.

Aidha mashuhuda wa tukio hilo wanaeleza kuwa moto huo ulishika kasi kwa haraka kutokana na hali ya hewa kuwa ya upepo mkali licha ya juhudi za wananchi kuuzima lakini uliwashinda nguvui hadi pale kikosi cha zima moto kutoka nchini Zambia kilipo fika na kuuzima moto huo.
Mwisho.


0 Responses to “ MOTO WATEKETEZA MADUKA MJINI TUNDUMA.”

Post a Comment

More to Read