Sunday, April 19, 2015

MAPICHAZI YA SIMBA WALIVYOCHINJWA NA MBEYA CITY BILA HURUMA SOKOINE

















(Picha na david Nyembe wa Fahari News)
WEKUNDU wa Msimbazi Simba wamefungwa magoli 2-0 na Mbeya City katika mechi ya ligi kuu soka Tanzania bara iliyochezwa uwanja wa Sokoine Mbeya jioni ya leo.

Kwa matokeo hayo Simba imeendelea kubaki nafasi ya tatu kwa pointi zake 35 baada ya kucheza mechi 22 nyuma ya mabingwa Azam fc wenye pointi 42  baada ya kushinda mechi yao leo mabao 2-1 dhidi ya Kagera.Azam nao wamecheza mechi 22. 

Vinara bado wanabaki kuwa Yanga kwa pointi 46 baada ya kucheza mechi 21.

Magoli ya Mbeya City yalifungw ana Paul Nonga dakika ya 45 kipindi cha kwanza akipokea pasi kutoka kwa Deus Kaseke.
City walifunga goli la pili dakika ya 69 kupitia kwa Peter Mwalyanzi. 

Simba ilipata pigo dakika ya 23 baada ya beki wake na nahodha, Hassan Isihaka kuumia na nafasi yake kuchukuliwa na Mganda Joseph Owino

0 Responses to “MAPICHAZI YA SIMBA WALIVYOCHINJWA NA MBEYA CITY BILA HURUMA SOKOINE”

Post a Comment

More to Read