Tuesday, April 28, 2015
KUHUSU TUHUMA ZA KUMDHURU DKT MENGI, IKULU YATOA NENO
Do you like this story?
Ikulu imekana
kuwepo kwa njama zozote za kutaka kumdhuru mwenyekiti mtendaji wa IPP LIMITED,
DK. REGINALD MENGI, zilizodaiwa kuandaliwa na Rais Jakaya Kikwete, kwa kile
kilichodaiwa kuwashughulikia wanaoihujumu serikali yake na kupanga
kumshughulikia baada kustaafu.
Habari hizo ziliripotiwa na gazeti la TAIFA IMARA ambazo
zilikuwa na kichwa cha habari ZITTO AMCHONGEA MENGI KWA JK na kudai kunasa
mazungumzo kati ya Rais Kikwete na kiongozi wa chama cha ACT-WAZALENDO, Zitto
Kabwe ambaye kwa wakati huo alikuwa Mwenyekiti wa PAC, ambaye inadaiwa
alimchongea kwake kwamba, ndiye kinara anayesababisha serikali yake iyumbe kila
mara.
Mkurugenzi wa mawasiliano ya Rais,Ikulu, Salvatory Rweyemamu,
amewaeleza wandishi wa habari jijini dar es salaam kuwa Rais aliposikia habari
hizo akiwa nje ya nchi alishtushwa nazo na kwamba Rais hawezi kushiriki njama
za kumdhuru raia na kuongeza kuwa habari hizo ni za kutengenezwa kwa nia mbaya
ya kuharibu uhusiano mzuri uliopo kati ya Rais na Dk. Mengi.
Akizungumzia suala la Rais kusaini au kutokusaini miswada
mbalimbali iliyopitishwa na bunge ukiwemo wa takwimu na makosa ya mtandaoni
ambazo baadhi ya wadau wa habari na tasisi mbalimbali zimekuwa zikimsihi Rais
asisaini hadi zifanyiwe marekebisho Rweyemamu amesema Rais atasaini yote kwani
ilipitia taratibu zote.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “KUHUSU TUHUMA ZA KUMDHURU DKT MENGI, IKULU YATOA NENO ”
Post a Comment