Tuesday, April 28, 2015
ZAIDI YA 4000 WATHIBITISHWA KUFA NEPAL.
Do you like this story?
Utawala nchini Nepal
unasema kuwa watu zaidi ya watu 4000 wamedhibitishwa kuaga dunia huku wengine
8000 wakijeruhiwa kwenye janga la tetemeko la ardhi lililosababisha uharibifu
mkubwa siku ya Jumamosi.
Jitihada za uokoaji zinaendelea kukiwa na
matumaini ya kuwapata manusura, lakini jitihada hizo bado hazijayafikia maeneo
mengine yaliyo mbali.
Watu wengi walilala nje kwa usiku wa tatu
mfululizo kwenye mji mkuu Kathmandu wakihofia kutokea kwa mitetemeo mingine
midogo.
Serikali ya Nepal inasema kuwa inahitaji kila
msaada ukiwemo wa mablanketi , helkopta, madaktari na madereva. Kuna uhaba wa
maji , chakula na umeme huku kukiwa na hofu ya kutokea kwa milipuko ya
magonjwa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ZAIDI YA 4000 WATHIBITISHWA KUFA NEPAL.”
Post a Comment