Wednesday, April 29, 2015
WAZAZI NA WALEZI MBEYA WATAKIWA KUSHIKAMANA NA WALIMU KATIKA MALEZI YA VIJANA.
Do you like this story?
Mwenyekiti wa Uvccm Mbeya Aman Kajuna akivishwa skafu na vijana wa skauti katika mahafali ya sita ya shule ya sekondari ya usongwe Mbalizi Wilayani Mbeya April 28 mwaka huu. |
Wahitimu wa kidato cha sita katika mahafali ya sita ya shule ya sekondari usongwe Mbalizi Mbeya wakifurahia katika mahafali hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa ushule hiyo April 28 mwaka huu. |
wanafunzi wa shule ya sekondari ya Usongwe Mbalizi wakiimba wimbo wa pamoja katika mahafali ya sita ya kidato cha sita yaliyofanyika shuleni hapo April 28 mwaka huu. |
Mwenyekiti wa Uvccm Mkoa wa Mbeya Amani Kajuna akizungumza katika mhafali ya sita ya kidato cha sita katika shule ya sekondari Usongwe Mbalizi wilaya ya Mbeya |
Picha ya pamoja mgeni rasmi Ndugu Amani Kajuna mwenyekiti wa Uvccm Mkoa wa Mbeya na wahitimu wa elimu ya kidato cha sita katika shule hiyo ya Usongwe Mbalizi April 28. |
Na Mwandishi wetu,Mbeya
Wito
umetolewa kwa Wazazi na walezi Mkoani Mbeya kuhakikisha wanatenga muda wao kwa
kukaa na vijana wao katika kuwajengea maadili mema badala ya kuwa tupia jukumu
hilo walimu pekee.
Kauli
hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha mapinduzi(UVCCM),
Mkoa wa Mbeya, Ndugu Aman Kajuna katika mahafali ya 6 kidato cha sita katika shule ya sekondari ya
Usongwe Mbalizi wilaya ya Mbeya.
Kajuna
amesema wazazi wengi wanafikiri kumaliza kulipa ada bila kufuatilia maendeleo
ya mtoto amekuwa ametimiza wajibu wake jambo ambalo sio sahihi kwani kuna
baadhi ya watoto ni wadanganyifu hawafiki shule hivyo ni wajibu wa mzazi
kufuatilia mwenendo wake.
Amesema
malezi ya mtoto yanatakiwa kuanzia nyumbani ba Kuhusu changamoto zilizotolewa
na Shule hiyo, Kajuna alisema kutokana na wingi wa wanafunzi ulivyo suala la
usafiri wa shule linapaswa kupewa kipaumbele cha pekee ili aweze kulitatua
hilo.
Ameema
endapo wazazi watashiriki kikamilifu katika malezi ya watoto kwa kufuatilia
nyendo zao kama wanahudhuria masomo kikamilifu itasaidia kuongeza ufaulu kwa
mwanafunzi pale atakaoona anafuatiliwa kwa ukaribu kila kona
Kwa
upande wake mkuu wa shule hiyo Ndugu Benedict Mahenge ametoa sababu mbalimbali
zinazofanya wanafunzi washindwe kufanya vyema katika masomo yao.
Mahenge
alisema shule hiyo haina ufaulu mzuri kwa wanafunzi wake hali inayotokana na
wazazi kuwaachia jukumu la kuwalea wanafunzi walimu pekee wakisahau kuwa suala
la malezi ya watoto linategemea pande zote mbili.
Amesema
changamoto kubwa ni wazazi kushindwa
kuwa karibu na watoto wao hali hiyo imesababisha kati ya wanafunzi 80 waliokuwa
wamechaguliwa kujiunga kidato cha tano 2013, 57 pekee wamefanikiwa kuhitimu
kidato cha sita mwaka huu huku 23 hawajulikani walikoishia.
Amesema
changamoto nyingine ni upungufu wa
walimu wa hesabu, upungufu wa vitabu, majengo muhimu kama bwalo la chakula
ambapo wanafunzi hulazimika kulia mabwenini jambo ambalo ni hatari.
Aidha
kutokana na changamoto hizo Mgeni rasmi katika mahafali hayo Mwenyekiti wa
Uvccm Mkoa wa Mbeya Ndugu Amani Kajuna alisema itabidi akutane na Mkuu wa Shule
ili waangalie uwezekano wa kupata gari litakalosaidia kulahisisha na kupunguza
changamoto zinazowakabili wanafunzi pindi dharula kama kuugua linapojitokeza.
Mwisho.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “WAZAZI NA WALEZI MBEYA WATAKIWA KUSHIKAMANA NA WALIMU KATIKA MALEZI YA VIJANA.”
Post a Comment