Sunday, May 3, 2015

SIMBA YAICHAPA AZAM 2-1 TAIFA, YAFUFUA MATUMAINI YA KUSHIRIKI MICHUANO YA KIMATAIFA MWAKANI




Wekundu wa Msimbazi SC, leo wamefufua upya matumaini ya kushiriki katika michuano ya kimataifa mwakani mara baada ya kuwafunga wana lambalamba timu ya Azam FC kwa jumla ya magoli 2-1, mchezo uliopigwa katika dimba la taifa jijini Dr es Salaam.

Kwa matokeo hayo Simba wamejiwekea kibindoni alama 44 huku wakiwa wamecheza michezo 25 na Azam wana alama 45 wakiwa wamecheza michezo 24.

Vita hii inaonekana kuwa ngumu sana baina ya timu hizi mbili huku kila timu ikionekana kuitolea macho nafasi ya pili baada ya Yanga kutangazwa mabingwa wapya msimu huu mara baada ya kujikusanjia pointi 55 katika michezo 24 waliyocheza ambapo si Azam wala Simba watakaoweza kuzifikia.

Azam watajilaumu kwa kupoteza mchezo wa leo kutokana  na kiungo wake mahiri Salum Abubakar ‘Sure Boy’ kutolewa nje kwa kadi nyekundu mara baada ya kumchezea madhambi beki wa kushoto wa Simba Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ katika dakika ya 38.

Simba walijipatia mabao yao kupitia kwa Ibrahim Hajib dakika ya 48 mara baada ya kupokea krosi maridhawa kutoka kwa kiungo mahiri wa timu hiyo kinda Said Ndemla , huku Ramadhan Singano 'Messi' akishindilia Msumari wa mwisho golini kwa Azam mnamo dakika ya 75 baada ya kuachia shuti kali lililomshinda mlinda mlango wa Azam, wakati wana lamba lamba Azam walijipatia goli lao kupitia kwa kiungo wao Mudathir Yahya mnamo dakika ya 57 kutokana na pasi nzuri aliyoipata kutoka kwa Kipre Tchetche.

Kwa matokeo haya, Simba wanatakiwa kushinda mchezo wao wa mwisho huku wakiiombea Azam ipoteze michezo yake miwili iliyosalia, ambapo itacheza na Yanga na baadaye kumalizia na wanajeshi wa Mgambo JKT kutoka
mkoani Tanga
Simba SC ; Ivo Mapunda, Hassan Kessy, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Joseph Owino, Juuko Murusheed, Jonas Mkude, Ramadhani Singano ‘Messi’/William Lucian ‘Gallas’ dk85, Said Ndemla/Elias Maguri dk75, Ibrahim Hajib, Emmanuel Okwi na Awadh Juma.

Azam FC; Aishi Manula, Shomary Kapombe, Gardiel Michael, Agrey Morris, Serge Wawa/Mudathir Yahya dk46, Himid Mao, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Frank Domayo/ Brison Raphael dk45, Didier Kavumbagu/John Bocco dk77, Kipre Tchetche na Brian Majwega.

0 Responses to “SIMBA YAICHAPA AZAM 2-1 TAIFA, YAFUFUA MATUMAINI YA KUSHIRIKI MICHUANO YA KIMATAIFA MWAKANI”

Post a Comment

More to Read