Monday, May 4, 2015

CHELSEA MABINGWA WAPYA LIGI KUU ENGLAND.






Timu ya Chelsea imeibuka mabingwa wa ligi kuu ya England, baada ya kuifunga Crystal Palace bao 1-0 katika mchezo uliofanyika katika uwanja wa Stamford Bridge. Bao la Chelsea lilifungwa katika dakika ya 45 ya kipindi cha kwanza cha mchezo, likifungwa Eden Hazard.

Chelsea ilihitaji pointi tatu kutangazwa mabingwa wa ligi kuu ya England. Chelsea imetwaa ubingwa huo ikiwa bado na michezo mitatu, ikiwa imejikusanyia pointi 83 ikifuatiwa na mabingwa wa msimu uliopita Manchester City yenye pointi 70, huku Arsenal ikiwa katika nafasi ya tatu na pointi 67 na nafasi ya nne inakaliwa na Manchester United yenye pointi 65.

Karibu timu zote za ligi hiyo ikiwa ni pamoja na nne za juu zimecheza michezo 35, isipokuwa Arsenal yenye michezo 33.
Jose Mourinho, kocha wa Chelsea
Ubingwa huo umemfanya kocha wa Chelsea Jose Mourinho ajisikie furaha, ajivune na kujisikia mchovu baada ya kazi ngumu ya kusaka taji hilo.

Ushindi huo umempa Mourinho ubingwa mara tatu akiwa kocha wa Chelsea, na kombe lake la kwanza akiwa kocha wa Chelsea mara baada ya kurejea mara ya pili kukiongoza kikosi hicho smimu uliopita. Hili ni taji la tano kwa klabu hiyo na limekuja miaka mitano baada ya timu hiyo kuchukua kombe lake la mwisho na ni miaka 60 tangu wachukue kombe la kwanza.

Shangwe na shamra shamra zilitanda kuzunguka eneo la Stamford Bridge baada ya filimbi ya mwisho kupulizwa. Kwa hakika Chelsea ilistahili kutwaa kombe hili kutokana kasi waliyoweka tangu kuanza kwa msimu wa ligi hiyo.

Ligi ikielekea ukingoni timu za Sunderland, QPR na Burnley ndizo ziko katika hatari zaidi ya kureremka daraja. Hata hivyo hali si shwari pia kwa timu za Leicester, Hull, Newscastle na Aston Villa

0 Responses to “CHELSEA MABINGWA WAPYA LIGI KUU ENGLAND.”

Post a Comment

More to Read