Thursday, May 7, 2015
UINGEREZA YAPIGA KURA LEO.
Do you like this story?
Mamilioni ya watu
watakuwa wakipiga kura katika uchaguzi mkuu wa Uingereza leo Alhamisi
Vituo vya kupigia kura karibu 50,000 nchini
kote vitafunguliwa saa moja asubuhi kwa saa za Uingereza.
Jumla ya wabunge 650 watachaguliwa kuingia
bunge la nchi hiyo, kukiwa na watu karibu milioni 50 waliojiandikisha kupiga
kura.
Kama ilivyo kwa uchaguzi mkuu, kuna viti
zaidi ya 9,000 vya madiwani vinavyogombewa katika serikali za mitaa 279.
Mameya pia watachaguliwa katika miji ya
Bedford, Copeland, Leicester, Mansfield, Middlesbrough na Torbay.
Hii ina maana kuwa karibu kila mpiga kura wa
England, ukiondolewa mji wa London ambako hakuna uchaguzi wa serikali za mitaa,
atapewa karatasi mbili za kupigia kura watakapofika katika kituo cha uchaguzi.
Baadhi ya kura tayari zimekwishapigwa kupitia
vituo vilivyoko nje ya Uingereza kwa kutuma kura kwa njia ya posta. Kura hizi
zilikuwa ni asilimia 15% ya kura zilizopigwa katika uchaguzi mkuu wa 2010
wakati watu waliojitokeza walikuwa asilimia 65%.
Masanduku ya kupigia kura yamepelekwa katika
vituo vya uchaguzi.
Kwa mara ya kwanza, watu waliweza
kujiandikisha kupiga kura kupitia njia ya mtandao.
Vituo vingi vya kupigia kura viko katika
majengo ya shule, kumbi za vituo vya kijamii na kwenye kumbi za parokia, lakini
migahawa, maeneo ya kufua na kunyosha nguo na basi la shule pia vitatumika kama
vituo vya kupigia kura.
Vituo vya kupigia kura vitafungwa saa nne
usiku kwa saa za Uingereza, lakini maafisa wa uchaguzi wamesema mtu yeyote
ambaye atakuwa kwenye mstari kufikia wakati huo ataweza kupiga kura yake.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “UINGEREZA YAPIGA KURA LEO.”
Post a Comment