Thursday, May 7, 2015

MADEREVA 15 WA MABASI NA DALADALA WATIMULIWA KAZI NA WAMILIKI WA MABASI HAYO KUTOKANA NA KUJIHUSISHA NA MGOMO.




Siku moja baada ya mgomo wa madereva kumalizika madereva 15 wa daladala na mabasi makubwa wamesimamishwa kazi na wamiliki wa mabasi hayo kwa madai ya kujihusisha na mgomo huo.

Katibu wa chama cha madereva BW RASHID SALEHE ametoa taarifa hiyo jijini dar es salaam ambapo amesema madereva 18 wamefikishwa mahakamani huko mkoani dodoma na kuongeza kuwa endapo wangekuwa na mikataba wanayopigania hivi sasa wasingefukuzwa kazi kienyeji namna hiyo.

Akizungumzia kamati iliyoundwa na serikali kushughulikia suala hilo baada ya mkuu wa wilaya ya kinondoni kuwaahidi kuwa ile iliyoundwa na waziri mkuu itafanyiwa maboresho wamesema hawana imani nayo baada ya idadi ya wamiliki ambao ndiyo wanaowalalamikia kuwa kubwa zaidi yao.

Madereva hao wana madai ya msingi matano ambayo ni pamoja na mikataba bora ya kazi, faini za mara kwa mara hata kwa kosa linalohitaji onyo, ukaguzi uliopitiliza, kwenda kusoma kila baada ya leseni kuisha muda wake na mwendo wa kilomita 80 kwa saa  madai yaliyosababisha mgomo uliotikisa nchi.

0 Responses to “MADEREVA 15 WA MABASI NA DALADALA WATIMULIWA KAZI NA WAMILIKI WA MABASI HAYO KUTOKANA NA KUJIHUSISHA NA MGOMO.”

Post a Comment

More to Read