Sunday, July 12, 2015

SALASALA VISION GROUP WAKABIDHIWA HATI ZA HEKARI 250 HUKO FUKAYOSI BAGAMOYO



Afisa Mtendaji Mkuu EAG Group Iman Kajula Wa Pili (kushoto) akipokea hati ya Kimila ya eneo walillonunua bagamoyo kwajili ya Jumuiya hiyo. Jumuiya iliyoasisiwa na wakazi wa Kilima hewa Salasala jijini Dar es salaam likiwa na malengo ya kijamii na kiuchumi. Tangu kuasisisiwa SVG imetekeleza miradi Mingi kwenye eneo la Salasala ikiwemo kupanda miti zaidi ya 5,000, kutengeneza barabara, kutengeneza viwanja vya michezo na kulinda maeneo ya wazi, Ulinzi, kutengeneza gari la polisi na misaada ya miradi mbalimbali endelevu ikiwamo kujenga ofisi ya Serikali ya Mtaa Salasala

SVG haikuishia hapo, imeamua kwa dhati kuchochea maendeleo ya Wanachama wake. Mradi mkubwa uliotekelezwa ni pamoja na kununua hekari 250 huko Fukayosi Bagamoyo. Baada ya ununuzi huu mchakato wakupata hati ulifanywa na kufanikiwa kupata hati za kimila na kukabidhiwa kwa wanachama wa SVG ili kuanza kuendeleza maeneno hayo.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Afisa Aridhi wa Wilaya ya Bagamoyo Bw.Kibona aliipongeza SVG kwa kuwa kikundi kilicho makini na kutumia dhima ya umoja ni nguvu, alisema hati za kimila zina faida nyingi sana ikiwamo kutokuwa na kipindi cha ukomo ikilinganishwa na hati za kawaida.
 Kwa upande wake, Mwenyekiti wa SVG Yahaya Banka alisema ‘’ SVG inalenga kuendelea kuwa chachu ya maendeleo kwa wanachama wake na familia zao. Tunaamini kwa kutumia nguvu ya umoja tunaweza kuleta maendeleo makubwa katika eneo letu tunaloishi pia kwa familia za wanachama’’

0 Responses to “SALASALA VISION GROUP WAKABIDHIWA HATI ZA HEKARI 250 HUKO FUKAYOSI BAGAMOYO”

Post a Comment

More to Read