Thursday, September 3, 2015
MTUMBWI WAZAMA ZIWA VICTORIA NA KUUA HARAMU.
Do you like this story?
Watuhumiwa watatu wa uvuvi haramu
wamekufa baada ya mtumbwi waliokuwa wakisafiria kuzama katika Ziwa Victoria
wakati wakipelekwa kituo cha polisi na askari waliowakamata.
Katika tukio hilo, bunduki ya kivita
aina ya AK-47 yenye namba 30900 pia ilizama ziwani na askari wa kikosi maalum
cha wapiga mbizi kutoka kitengo cha Marine na Bandari kulazimika kufanya kazi
ya ziada kuiopoa majini.
Ajali hiyo ilitokea juzi baada ya
mtumbwi huo kupigwa na dhoruba kali.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Joseph
Konyo, alithibitisha tukio hilo lilitokea Agosti 18, mwaka huu, wakati askari
hao walipokuwa wakisafiri na watuhumiwa hao katika mtumbwi uliozama wakati
wakiwapeleka Kituo cha Polisi Kageye.
Aliwataja waliokufa katika tukio hilo
kuwa ni, Dioniz Masatu (26), Revocatus William (26) na Stadius Audaxi (23),
wote wakazi wa kjiji cha Kazilatemwa, wilayani Muleba na walionusurika ni
Shabaan Maiga (45) na Fikiri Mafulu (46) ambao walijiokoa kwa kuogelea.
Kamanda Konyo alisema askari mmoja wa
hifadhi aliogelea umbali wa zaidi ya mita 800 na kujiokoa, huku mwingine
akishikilia mtumbwi uliopinduka na baadaye kuokolewa kabla haujazama.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ MTUMBWI WAZAMA ZIWA VICTORIA NA KUUA HARAMU.”
Post a Comment