Monday, October 5, 2015
SIRI IMEFICHUKA MTIKILA AMEUAWA.
Do you like this story?
Na Mwandishi Wetu
KIFO cha Mchungaji Christopher Mtikila (65) aliyezaliwa
mwaka 1950, kimezua utata ambapo baadhi ya watu wa karibu na mwanasiasa huyo
wanadai kwamba ‘ameuawa’.
Akizungumza kwa sharti la kutotajwa jina lake gazetini,
mmoja wa watu hao amesema licha ya Jeshi la Polisi nchini kusema kwamba kifo
hicho kilichotokana na ajali iliyosababishwa na mwendo kasi, lakini kuna kila
dalili za ‘mkono wa mtu’ kutokana na harakati za mwanasiasa huyo katika masuala
ya kijamii, kitaifa na kimataifa.
Mchungaji Mtikila, Mwenyekiti wa Chama cha DP na kiongozi wa
kanisa la Full Salvation, alifariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea usiku
wa kuamkia jana Jumapili Oktoba 4, 2015 katika Kijiji cha Msolwa mkoani Pwani
wakati akitokea Morogoro.
“Hatuwezi kuridhika kwamba ni ajali tu, lakini tunaliomba
Jeshi la Polisi lifanye uchunguzi wa kina kuhusiana na kifo hicho, kwani kuna
mashaka makubwa kwamba huenda ameuawa kabla ya ajali hiyo kutokea kutokana na
mambo ambayo Mchungaji alikuwa akiyafuatilia kwa muda mrefu,” alisema mtu huyo
wa karibu na Mtikila.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Jaffar Mohammed, amelieleza
Ijumaa Wikienda kwamba, ajali hiyo ilitokea majira ya saa 11:45 alfajiri ambapo
gari hilo aina ya Toyota Corolla Namba T 189 AGM lilikuwa likiendeshwa na
George Steven ‘Ponera’ (31), mkazi wa Mbezi, Dar ambapo chanzo chake ni mwendo
kasi uliosababisha gari kuacha njia na kupinduka.
Majeruhi
wengine mbali ya dereva wa gari hilo ni Mchungaji Patrick Mgaya (57) mkazi wa
Dar es Salaam na Ally Mohammed (42), mkazi wa Mbezi jijini Dar.
Chanzo chetu cha habari kinaeleza kwamba, kauli za hivi
karibuni za Mchungaji Mtikila kuhusu masuala ya ufisadi kwa baadhi ya wagombea
urais nchini Tanzania pamoja na siasa za kimataifa zinazohusisha mataifa jirani
nazo zinaweza kuwa chanzo na akaonya kwamba uchunguzi wake usiishie kujua
chanzo cha ajali ya gari.
Hata hivyo, kutokana na utata huo, tayari dereva wa gari
hilo, George Ponera anashikiliwa na polisi kwa mahojiano zaidi.
Chanzo:
Global publishers.co.tz
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ SIRI IMEFICHUKA MTIKILA AMEUAWA.”
Post a Comment