Monday, November 9, 2015

DUUH HII KALI: JAMAA ATUPWA JELA MIAKA 885




Najua tumeshawahi kukutana na stori kuhusu hukumu za kifungo cha miaka kadhaa mpaka 30 jela, au wengine wanahukumiwa kifungo cha maisha baada ya kufanya makosa mbalimbali… lakini kuna hukumu ambazo ukitajiwa namba za miaka yake unaona bora kama hukumu yenyewe ingekuwa tu kifungo cha maisha !! Miaka 885 jela, anatoka mtu kweli hapo ?!

Shawn Ryan Thomas alidakwa na Polisi Florida Marekani akiwa na picha za utupu za watoto wadogo, kesi ikafika Mahakamani na hukumu yake ikatolewa kwamba atatakiwa kutumikia jumla ya miaka 885 jela.

Ripoti nyingine kutoka  Florida Department of Law Enforcement imesema Thomasalinaswa pia akiwa kwenye mpango wa kumteka msichana mwingine mdogo, kuwaua wazazi wake na kumrekodi mkanda wa utupu !!
Stori yake iko kwenye Video pia mpaka Mahakama ilivyomsomea hukumu.


0 Responses to “ DUUH HII KALI: JAMAA ATUPWA JELA MIAKA 885”

Post a Comment

More to Read