Tuesday, December 22, 2015
ASILIMIA 49 YA WANAUME TANZANIA, SI WAZAZI HALALI WA WATOTO WAO
Do you like this story?
Asilimia 49 kati ya asilimia 100 ya matokeo
ya uchunguzi wa makosa ya vinasaba (DNA) yanayowasilishwa katika ofisi ya
Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa mwaka yanaonyesha kuwa baba si
mzazi halali wa mtoto katika kesi hizo.
Hayo yamesemwa na Mkemia Mkuu wa Serikali,
Profesa Samwel Manyele alipokuwa akiongea na waandishi wa habari mara baada ya
kufungua mkutano wa wadau wa wakala wa afya ya mazingira leo jijini Dar es
Salaam
Kesi zinazopokelewa katika maabara yetu
zinazohusu sampuli ya Vinasaba kwa mwaka zinaonyesha kuwa asilimia 49% kati ya
asilimia 100% ya matokeo hayo huonyesha mzazi mmoja ambaye ni baba kuwa si
mzazi halali wa mtoto huyo”.
“Vinasaba ni utambulisho wa kipekee wa kila
kiumbe ambao unabeba taarifa muhimu na inayorithisha tabia au umbile fulani la
mhusika. Vinasaba ni kama vile kitabu cha kumbukumbu kinachohusu maisha
binafsi”, aliongeza Prof. Manyele.
Profesa Manyele aliongeza kuwa mikoa ya kanda
ya Ziwa, Arusha, Dar es Salaam na Mbeya ndio inayoongoza kwa matokeo ya
uchanguzi huo wa makosa ya Vinasaba nchini.
Akizungumza kuhusu lengo la mkutano huo,
Profesa Manyele amesema kuwa ni kuimarisha uhusiano uliopo kati ya wadau wa kemikali
na wadau wa afya ya mazingira kutoka katika halmashauri tofauti nchini pamoja
na ofisi ya Mazingira.
Aidha Profesa alibainisha baadhi ya majukumu
yanayofanywa na wakala wa Mkemia Mkuu wa Serikali kuwa ni kufanya uchunguzi ili
kuhakiki ubora na usalama wa vyakula, dawa, maji, maji machafu, bidhaa za
viwanda na mashambani, sampuli za mazingira na sampuli zinazohusiana na makosa
ya jinai.
“Matokeo ya uchunguzi wa makosa ya jinai na
vinasaba (DNA) huviwezesha vyombo husika kufikia maamuzi stahili na kusaidia
kutendeka kwa haki katika tuhuma za kesi za jinai ikiwemo ulevi, mauaji,
ubakaji, wizi wa watoto, uhalali wa mtoto kwa mzazi, kwa kupitia vyombo husika”
alifafanua Profesa.
Mbali na hayo, alisema wakala kwa
kushirikiana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
inatarajia kuwasilisha mapendekezo ya kutunga sheria ya kuunda maabara ya
Mkemia Mkuu wa Serikali na Sheria ya kusimamia taaluma ya Wakemia, kuimarisha
upatikanaji wa mitambo na vifaa vya maabara kila teknologia inapobadilika
pamoja na kuimarisha zaidi taratibu za uchunguzi ziwe za kisasa ili kuendana na
mabadiliko ya sayansi na teknologia.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
.gif)


0 Responses to “ ASILIMIA 49 YA WANAUME TANZANIA, SI WAZAZI HALALI WA WATOTO WAO”
Post a Comment