Tuesday, December 22, 2015
ZAIDI YA HEKARI 150 ZA MAHINDI ZAFYEKWA WILAYANI MBOZI
Do you like this story?
Zaidi
ya hekari 150 za Mahindi zimefyekwa na watu wanaodaiwa kuwa ni askari wa idara
ya maliasili wilayani Mbozi na kusababisha wananchi zaidi ya 400 kuwa katika
hatari ya kukumbwa na uhaba wa chakula mwaka huu.
Wananchi wa
vijiji vya Nambizo, Utambalila na Ipapa katika kata ya Nambizo wilayani Mbozi
ndio ambao wameathirika na zoezi hilo la ufekaji wa Mahindi yao wakidaiwa
kulima kwenye hifadhi ya msitu wa Isalalo, hali ambayo imewafanya wananchi hao
kuishi kwa hofu ya kukumbwa na baa la njaa.
Uongozi wa
vijiji na kata ya Nambizo umelaani tukio hilo kwa madai kuwa askari hao
wamevamia kata hiyo na kufanya uharibifu wa mazao bila kushirikisha uongozi wa
serikali katika kata hiyo.
Mbunge wa jimbo
la Mbozi, Pascal Haonga ametembelea eneo la mashamba hayo na kujionea uharibifu
mkubwa wa mazao na kusema kuwa yeye kama mwakilishi wa wananchi hawezi kukaa
kimya hivyo atachukua hatua ya kuwaona viongozi wa juu serikalini kujua hatma
ya wananchi hao.
Wilaya ya Mbozi
ni miongozi mwa maeneo yanayozalisha Mahindi kwa wingi na kuiuzia serikali
kupitia wakala wa hifadhi ya chakula nchini kwa ajili ya kuwasaidia watanzania
katika maeneo mbalimbali nchini wanaopatwa na uhaba wa chakula.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
.gif)

0 Responses to “ZAIDI YA HEKARI 150 ZA MAHINDI ZAFYEKWA WILAYANI MBOZI”
Post a Comment