Tuesday, December 22, 2015
USHINDI WA ARSENAL DHIDI YA MAN CITY WAMPA KIBURI MZEE WENGER, MSIKIE ALICHOKISEMA
Do you like this story?
Ushindi walioupata Arsenal dhidi ya
Manchester City umewapa imani kuwa wapo kwenye mbio za kuwania ubingwa wa ligi
kuu England msimu huu, amesema manager wa klabu hiyo Arsene Wenger.
The Gunners hawajatwaa taji la ligi kuu
England tangu mwaka 2004, lakini magoli kutoka kwa Theo Walcott na Olivier
Giroud yalitosha kuimaliza City licha ya Yaya Toure kufunga goli pekee kwa
klabu yake dakika za lala salama.
“Inatufanya tujiamini, tunapata nguvu na
imani”, alisema Wenger.
“Sasa angalau kikosi chetu kinajielewa, kitu
ambacho unaweza kukiona wakati wa mchezo wakati tulipokuwa kwenye presha”.
Sasa Arsenal wako pointi nne mbele ya
Manchester City lakini bado wanasalia nafasi ya pili pointi mbili nyuma ya
vinara Leicester City.
Wakati huo mabingwa watetezi wakiwa nafasi ya
15 na wanaonekana wako nje ya kinyang’anyiro cha ubingwa cha kutwaa ubingwa wa
EPL huku nafasi kubwa wakipewa The Gunners.
Arsenal haijafungwa kwenye mechi sita
mfululizo na hiyo inatoa matumaini kwa kocha wa kikosi hicho mzee Wenger ambaye
anaamini msimu huu wanatakiwa kutwaa taji hilo walilolikosa kwa muda mrefu
sasa.
“Miaka miwili au mitatu iliyopita tulikaa
kileleni kwa muda mrefu lakini kitu special msimu huu ni kwamba, tumecheza bila
wachezaji wetu wengi muhimu, tulisafiri kuwafuta Olympiakos, tukacheza dhidi ya
Aston Villa na Man City lakini tumeshinda michezo yote”, amesema Wenger.
“Hicho ni kitu kizuri. Ninaimani kwamba
tumeonesha vipaji vyetu na ari pamoja na kiwango cha juu ambavyo vimetupa
pointi tatu”.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
.gif)


0 Responses to “USHINDI WA ARSENAL DHIDI YA MAN CITY WAMPA KIBURI MZEE WENGER, MSIKIE ALICHOKISEMA”
Post a Comment