Saturday, December 19, 2015
BAADA YA KUFUKUZWA MOURINHO, VAN GAAL AHOFIA KIBARUA CHAKE
Do you like this story?
Baada ya kocha Jose Mourinho kutupiwa virago
na klabu ya Chelsea, presha ni kubwa kwa kocha wa Manchester United Louis Van
Gaal ambaye anasema anahofia kibarua chake na kwamba hajui kwamba inaweza kuwa
ni zamu yake kuondoka kama hatopata matokeo haraka.
Van Gaal ambaye amesikitishwa kufukuzwa kazi
kwa kocha wake huyo msaidizi wa zamani wakiwa wote Barcelona, na kusema hawezi
kudadisi zaidi chanzo cha kufukuzwa kocha huyo aliyemzungumzia kuwa bora zaidi
wa kizazi chake na mwenye rekodi ya kipekee.
Kocha huyo amesema anahofia kumalizia career
yake ya ukocha kwa kufukuzwa na kwamba anahitaji kupata matokeo kuepusha hilo
mara baada ya kuenda mechi tano bila ushindi huku wakifungwa na Vfl Wolfsburg
na Bournemouth mfululizo.
Tayari wachambuzi wa soka duniani wanaona ni
wakati Manchester United inatakiwa kuachana na Louis Van Gaal na badala yake
kumnasa kocha Pep Guadiola ambaye anamaliza muda wake Bayern Munich ama Jose
Mourinho ambaye ni chaguo la mashabiki, huku ikielezwa pia kuwa bado Van Gaal
anapata sapoti kubwa kutoka katika bodi ya klabu hiyo.
Wakati huo huo, kocha Manuel Pellegrine wa
Manchester City akizungumzia sakata hilo amesema kuwa yeye binafsi hawezi
mkumbuka Jose Mourinho lakini akakiri kuwa ni pengo kubwa katika ligi kuu
England kutokana na uwezo wa mreno huyo. Pellegrine akiendelea zaidi amesema
katu hana presha yeyote ile pamoja na mazungumzo yanayoendelea hivi sasa ya
kumuhusu Gadiola kurithi mikoba yake msimu ujao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
.gif)


0 Responses to “BAADA YA KUFUKUZWA MOURINHO, VAN GAAL AHOFIA KIBARUA CHAKE”
Post a Comment