Wednesday, January 27, 2016
NETANYAHU AMSHUTUMU BAN KI-MOON
Do you like this story?
![]() |
Benjamin Netanyahu |
Waziri mkuu wa
Israel,Benjamin Netanyau amemshutumu katibu mkuu wa umoja wa mataifa,Ban
Ki-Moon kwa "kuunga mkono ugaidi", baada ya kusema kuwa ni jambo la
kawaida kwa watu wanaotawaliwa au kukandamizwa, kukabiliana na walowezi.
Bw Ban alikuwa akizungumzia mzozo wa
Wapalestina.
Zaidi ya Wapalestina 155, Waisraeli 28,
Mmarekani na Raia wa Eritrea wameuawa kwa kushambuliwa kwa risasi au kudungwa
visu tangu Oktoba.
"Matamshi ya katibu mkuu wa UN yanaunga
mkono ugaidi," alisema Bw Netanyahu kupitia taarifa.
"Hakuna haki kamwe kutetea ugaidi."
Akihutubia Baraza la Usalama la Umoja wa
Mataifa, Bw Ban alikuwa amesema visa hivyo vimeongezeka kutokana na kutamauka
miongoni mwa Wapalestina, na hasa vijana.
"Palestinian frustration is growing
under the weight of a half century of occupation and the paralysis of the peace
process," he said.
"Kama watu wanaokandamizwa
walivyoonyesha katika historia, ni kawaida kwa binadamu kukabiliana na
walowezi, jambo ambalo huchochea chuki na misimamo mikali," alisema Bw
Ban.
Alieleza kuwa hatua za usalama pekee haziwezi
kusitisha migogoro inayotishia amani.
Lakini kwa mujibu wa Bw Netanyahu,
Wapalestina wenyewe ndio wanaohujumu juhudi za kuundwa kwa taifa lao.
Aidha, amesema Umoja wa Mataifa ulipoteza
mwelekeo wake siku nyingi zilizopita.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ NETANYAHU AMSHUTUMU BAN KI-MOON”
Post a Comment